Mke wa Ulomi asimulia sakata la kupotea kwa mumewe

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Elizabeth Munisi ambaye ni Mke wa Mfanyabiashara aliyepotea tangu December 11,2024 Jijini Dar es salaaam, Daisle Simon Ulomi, ameiomba Serikali kupitia Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuendelea na uchunguzi huku pia akiwasihi Wadau wa Haki za Binadamu na Watanzania wote kuendelea kupaza sauti ili Mumewe apatikane akiwa mzima.

Soma, Pia: TRA: Hatuhusiki na kupotea kwa mfanyabiashara Daisle Simon Ulomi

Akiongea leo December 15,2024 Jijini Dar es salaam kwenye mahojiano maalum na Mwandishi wa AyoTV Bakari Chijumba, Mke wa Ulomi amesema "Tulitoka wote nyumbani tukaenda kwenye eneo letu la biashara Sinza Kijiweni, saa 6:00 mchana tukapigiwa simu na Wakala anayetusaidia kutoa mzigo wetu wa vifaa vya ujenzi kwa ajili ya nyumba yetu ambao umetoka China, Wakala akatuambia TRA wamefungua kontena wameona kuna vitu kama vioo kwahiyo wakati wanakagua watashusha baadhi ya vitu kwahiyo ili kujitoa kwenye shida mwenye mali awepo"

"Mumewe wangu akaondoka kuelekea Mbagala, Bandari kavu kwenda kukagua kontena hilo akitumia pikipiki namba MC 415 DQC aliyokuwa akiendesha mwenyewe, kufika saa tisa alasiri Wakala akanipigia kwamba hadi sasa hivi huyu Mumeo hajafika nikamwambia ameondoka saa mbili zilizopita alitakiwa awe amefika, nami nikapiga hakupatikana, hadi saa 12 jioni Wakala ananiambia naona leo imeshindikana nafunga hili kontena, tukaanza kuuliza kwa Rafiki zake hatukufanikiwa, tukazunguka vituo vya Polisi na Hospitali mbalimbali kwenye vyumba vya kuhifadhi maiti kwamba labda amepata ajali kote hatukumuona"
 
TRA kweli hapo hausiki...na ukiona mpaka mwenye mzigo unaitwa na TRA jua huyo agent wako maelezo yako hayajawatosheleza TRA kwenye ukaguzi basi watamuita mwenye mzigo kutoa maelezo!
Sasa swali la kujiuliza kama hajafika hapo kwenye bandari kavu kaishia wapi ?

Ova
 
Kama TRA hawahusiki, huyo wakala kuna kitu anaficha!...
 
View attachment 3177176
TRA na watekaji damu damu ...watekaji wana kazi mbalimbali serikalini
 
TRA kweli hapo hausiki...na ukiona mpaka mwenye mzigo unaitwa na TRA jua huyo agent wako maelezo yako hayajawatosheleza TRA kwenye ukaguzi basi watamuita mwenye mzigo kutoa maelezo!
Sasa swali la kujiuliza kama hajafika hapo kwenye bandari kavu kaishia wapi ?

Ova
Huyo Agent anajua kitu. Maana ndiye aliyetumika kumvuta kwa watekaji au labda kama aligongwa na kufariki .
 
Unaweza kuta hiyo simu ni yakujihami tu kwamba hawajaonana ila wameonana.

Lolote linawezekana, kwasasa hivi hawa mashkaji siwaamini pia.
investigation-discovery-logo.jpg
 
Back
Top Bottom