Mimi siziamini picha hizo kwa sababu zifuatazo:
1. Kitendo cha waziri huyo kuruhusu mkewe huyo kupigwa na huyo shemeji yake aliye kifua wazi.
2. Shemeji mtu mwenye jeans kama hakuwa ndani alitoka wapi kuja kumpiga wakati yupo kifua wazi au alimpiga wakati ameshavua shati, kitendo ambacho si rahisi
3. Hakuna hata picha moja hapo ya huyo aliyefumania, yaani Waziri.
4. Huyo mwanamke mwenye baibui wanasema kafumaniwa na alikua akizini, alijiremba saa ngapi na lipstick hiyo mdomoni baada ya kutokea tukio hilo lenye utata?
5. Sidhani kama kichwa cha huyo mwenye baibui ndiyo cha mwenye mwili huo
6. Anaonekana alipigwa picha akipata kibano kama ni sebuleni vile. Akaenda chumbani akavaa baibui akafuatwa tena huko na waandishi akawaruhusu wampige picha akiwa amekaa kwa huzuni hivyo.
Uzushi na uongo mtupu!