Mke wangu ana Mawasiliano na Mkwe na Mashemeji wa X wake. Pia ana account ya Social Network ambayo ameniblock siwezi kuiona anachoweka huko

Wewe hadi umeoa basi unaakili timamu.

unasema unampenda mkeo basi zidisha upendo ipo siku ataacha hayo mambo mkuu.

Ndoa sio mchezo mkuu...kuoa na kuacha unajitia GUNDU tu....

Tuliza akili itulie huwenda pia anakupima IQ yako inauwezo wa namna gani katika kufikilia.....ACHANA NA MHEMKO
 
Hapana Hana mtoto
Sawa sasa uzoefu wangu unaniambia hivi......
1. Huyo mkeo alikubali kuolewa na wewe kwasababu alihitaji harusi na sio ndoa.
2. Inavyo onekana mkeo bado anaupendo wa dhati kwa X wake na bado anamatarajio na mipango flani ya mbeleni kwenye familia ya X wake.
3. Kwa mtazamo wangu mimi huyo sio mke wako, bali unaishi na mke wa mtu.
4. Ulijikuta unaoa mwanamke ulie mpenda pasipo kujipa nafasi ya kumjua vizuri.
5. Nahisi unamadhaifu flani kwa mkeo na tayari amesha yagundua.

Ushauri wangu ni:-
Ingekua mimi ndio wewe, baada ya kupata ushahidi ulio jitosheleza wala nisinge hangaika kutafuta ushauri na nisinge waza mara mbili, bali ninge mpiga chini pasipo kujali maumivu yangu ama yake. Baada ya hapo ningezima masikio kwa maneno na mashambulizi yoote ambayo ningetupiwa na ndugu jamaa na marafiki.
Na mwisho kabisa nisinge kubali ushauri wa aina yeyote kutoka kwa mtu yeyote kwasababu hakuna kati yao ambae angenisaidia kuyabeba maumivu ambayo nimeyapata.
Mwisho kabisa, dalili ya mvua ni mawingu walisema wahenga.
 
Bila shaka huyu mke ni single mom.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…