Mke wangu ana tabia za wizi na udokozi

Kuna mwamba mkewe alikuwa anamwibia hasa akilewa, akabunu mbuni akawa akifika nje kwake anaficha hela nje kwenye maua kwenye wallet anaacha afu 5 tu. Shikamoo wanawake akausoma mchezo ikawa kazi bure akificha asubuhi hakuti kitu, akaweka mtego ndio akajua ni mkewe.
 
Hi labia wanayo wanawake wengi sana, na na ukimchunguza hapo atakua lazima ana mikopo ile ya vikundi aka. kaushadamu, jaribu kuongeza pocket money yake na usiweke cash nyumbani, hii labia inaweza kwenda mbali hata kuchukua vitu nyumbani kama vyakula.
 
Mwmbie hiyo tabia mbaya aache tabia za uswazi
 
Wizi ni tabia za kiubinafsi na mipango ya siri.....mwenza mwenye tabia ya wizi tafsiri yake ni mbinafsi na ana mipango mingine ya nje ya muunganiko wa ndoa.......

Kaa uzungumze na umueleweshe kama bado hiyo tabia inaendelea wewe mwenyewe utajua cha kufanya......

Mwanamke mwizi kwenye mfuko wa mumewe ni sawa na wewe unajenga halafu mwenzio anabomoa.......ni agharabu sana kupiga hatua na inapunguza upendo kwa wanandoa......
 
Hii kitu nishakihisi...mfano zamani nilikuwa nikinunua gunia la mkaa,linakaa hata miezi miwili,,, sasa hivi hata Mwezi haufiki vizuri gunia limeisha
 
Mpe hela za kutosha ataacha wizi, tatizo lako humpi hela za kutosha. Ubahiri tu.
 
Inaudhi sana tena sana, si uombe!
 
Kweli kabisa ndugu,,, Kuna wakati Ile Hela kwenye wallet Ina mipango ya kifamilia,,,mwenzio anakurudisha Nyuma kumuubia mumewe,,,
 
Ndani ya miaka mitatu alikuwa mwizi ama ni tabia mpya

Sema mke na mume ni mwili mmoja...chako ni chake so logically ni "amechukua" 🥴
Kwahiyo na mume aanze tabia za udokozi, mbugi yake vikao vya familia hadi vitahusishwa...


Mimi nadhani jamaa labda aachi pesa ya matumizi ya uhakika.. ni vizuri akakaa naye na kuona sababu hasa ni nini. Kuna mahitaji mwanamke anapaswa kuyatimiza nje na pesa ya kula ni ngumu kuomba kwa mume ikiwa mke hana chanzo cha mapato..
 
Na mimk mkuu mke wangu ana tabia hizo hizo Moderator unganisheni uzi na mimi pia mke wangu kama wa jamaa
 
Alijisevia marejesho ya vicoba.Kuwa na amani mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…