Mke wangu ana tatizo la kukoroma

luis diaz

Member
Joined
Feb 28, 2022
Posts
86
Reaction score
208
Kwema wadau?

Mke wangu amekua ana tatzo la kukoroma haswaa anakoroma utafirikiri mwanaume hii hali ya kukoroma ina tibika kweli

Msaada kwenu
 
Inaweza ikawa ni moja ya sababu,ila nawengine watachangia sababu nyinginezo,mimi nilikua na tatizo hilo ila baada ya kukata kilimi niko fresh kabisa
Sawa asante leo nimeongeza kitu kichwani!
 
Afanye hili zoezi mara 5-10 Kwa siku


1. PanuA mdomo Hadi mwisho Kwa nguvu ,

2. Atoe ulimi nje Kwa nguvu Hadi mwisho

3. Wakati mdomo uko wazi awe anautoa ulimi nje na ndani Kwa nguvu , utaona Hadi machozi yanamtoka.

Afanye hili zoezi , utakuja kunishukuru. Hili zoezi linakomaza misuli iliyolegea nyumA ya ulimi ambayo ndio husababisha MTU kukoroma
 
Inatibika kwa:-

1. Kukata kimeo

2. Kufuata maelekezo hapo juu.

3. Ongeza Upendo

4. Apunguze Unene

5. Akilala aweke mto. Alalie mto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…