Mke wangu anamtesa sana mtoto wa marehemu dada yangu

Kama mjuavyo sisi wanaume mara nyingi ni kuamka asubuhi na mapema na kuondoka, na kurudi ni usiku, muda ambao Mimi nashinda nyumbani ni Jumamosi na Jumapili.

Usiku wa kuamkia Jana alhamis mtoto wa marehemu dada yangu alianza kulia sana chumbani, akalia sana mpaka ikabidi niamke niende chumbani kwao Ili nione Kuna nini, nilivyo fika nilimkuta kakaa chini huku wenzie wamelala, nikamwuliza Kuna nini? Akanijibu mguu unamuuma sana, ikabidi niuangalie mguu, aisee nilijikuta nalia na Mimi, mguu ulikuwa umevimba sana, nikamwuliza ilikuwaje? Akaniambia mke wangu alimpiga na kipande Cha tofali.

Pale pale nikaenda kumwamusha mke wangu kumwuliza hiki alicho fanya, akawa amekataa na kuanza kumfokea mtoto eti anataka kutugombanisha, Nikasema sawa, ila kwanini mguu unafikia hatua hii ina maana alikuwa hamuoni? Akawa amezidisha hasira eti natafuta sababu kama nime mchoka niseme arudi kwao, nikaona maneno yasiwe mengi ikabidi nimpakie mtoto kwenye gari nikampeleka hospital usiku ule ule, iligundulika kuwa mfupa wa mbele wa mguu uliachia kidogo akafungwa P.O.P.

Nilivyo rudi nyumbani asubuhi Jana hiyo asubuhi ilibidi nishinde nyumbani, ikabidi nifanye upelelezi mana Kuna vitu niliiona haviko sawa, ndo mpangaji wangu mmoja akaniambia kama Kuna sehemu naweza kumpeleka huyu mtoto Bora nimpeleke vinginevyo itatokea hatari kubwa, mtoto anateswa mno na mara nyingi shuleni haendi, na siku alivyo mpiga na tofari alikuwa amemtuma vitafunwa asubuhi akachelewa kurudi, tofari alimpiga mbele ya wapangaji siku tatu nyuma, na siku zote hizo hakwenda shule.

Nawaza mtoto nimpeleke wapi, marehemu dada yangu baada ya kufariki 2022 tuligawana watoto sisi ndugu zake, hili tukio limefanya nimkumbuke marehemu dada yangu aliye fariki Kwa maumivu makubwa ya kansa akiwa mikononi mwangu, nawaza Bora kuachana na mke wangu kuliko kuacha mtoto wa dada ateseke ntakuwa nimemkosea dada.

Mke wangu alimchukua mtoto wa kaka yake anaishi hapa na anaelekea kumaliza form 4 Kwa Gharama zangu, ila mtoto wa upande wangu kashindwa kumlea Kwa miaka miwili tu,hii ni sawa kweli?

Halafu baada ya mtoto kuniambia kuwa yeye ndo alimpiga, muda wote saivi ni kumuangalia Kwa jicho Kali sana na kumwambia eti ametumwa aje kutugombanisha, mtoto wa miaka 8 anawezaje kutugombanisha?

Sikuwahi kumfikiria mke wangu kuwa anaweza fanya hiki alicho fanya kutokana na mambo ninayo wafanyia ndugu zake, na ndiyo maana huyu mtoto nilimleta hapa Kwa kuamini atamsimamia kama mwanae na kama anavyo wasimamia watoto wetu wawili.

Mpaka naogopa kwenda kazini na huyu mtoto kumuacha hapa, nahisi atampiga Yani

Daah wanaume wanazid kupungua aisee. Uko serious kabisa mkuu? Kwa kifupi huyo mkeo hakufai. Huyu ukiishiwa au ukianza kuzeeka utafute pa kuishi ni shetan, mpige chini Nimeumia sana daa
 
Inasikitisha sana kwakweli kwamba mtu amekosa namna ya kumuadhibu mtoto mpaka anamponda na kipande cha tofali as if anapiga mwizi...

Halafu sijui kwanin tu hizi domestic violence zinazopigiwa kelele ni zile za mwanaume kumpiga mwanamke tu.... ni nadra sana kusikia hao wanaharakati wenu wakipigia kelele unyanyasaji unaofanywa na wanawake kwa watoto.
Umeona enh!
Yan nawaza tofali, alikuwa anaua nyoka? aiseeeh
 
hivi umejitafakari siku ukiishiwa ama ukapata ulemavu au matatatizo ya muda mrefu atakutreat vipi huyo mkeo??? tatizo mnaoa kwa vigezo vya sura na matako ona sasa...
 
Kama mjuavyo sisi wanaume mara nyingi ni kuamka asubuhi na mapema na kuondoka, na kurudi ni usiku, muda ambao Mimi nashinda nyumbani ni Jumamosi na Jumapili.

Usiku wa kuamkia Jana alhamis mtoto wa marehemu dada yangu alianza kulia sana chumbani, akalia sana mpaka ikabidi niamke niende chumbani kwao Ili nione Kuna nini, nilivyo fika nilimkuta kakaa chini huku wenzie wamelala, nikamwuliza Kuna nini? Akanijibu mguu unamuuma sana, ikabidi niuangalie mguu, aisee nilijikuta nalia na Mimi, mguu ulikuwa umevimba sana, nikamwuliza ilikuwaje? Akaniambia mke wangu alimpiga na kipande Cha tofali.

Pale pale nikaenda kumwamusha mke wangu kumwuliza hiki alicho fanya, akawa amekataa na kuanza kumfokea mtoto eti anataka kutugombanisha, Nikasema sawa, ila kwanini mguu unafikia hatua hii ina maana alikuwa hamuoni? Akawa amezidisha hasira eti natafuta sababu kama nime mchoka niseme arudi kwao, nikaona maneno yasiwe mengi ikabidi nimpakie mtoto kwenye gari nikampeleka hospital usiku ule ule, iligundulika kuwa mfupa wa mbele wa mguu uliachia kidogo akafungwa P.O.P.

Nilivyo rudi nyumbani asubuhi Jana hiyo asubuhi ilibidi nishinde nyumbani, ikabidi nifanye upelelezi mana Kuna vitu niliiona haviko sawa, ndo mpangaji wangu mmoja akaniambia kama Kuna sehemu naweza kumpeleka huyu mtoto Bora nimpeleke vinginevyo itatokea hatari kubwa, mtoto anateswa mno na mara nyingi shuleni haendi, na siku alivyo mpiga na tofari alikuwa amemtuma vitafunwa asubuhi akachelewa kurudi, tofari alimpiga mbele ya wapangaji siku tatu nyuma, na siku zote hizo hakwenda shule.

Nawaza mtoto nimpeleke wapi, marehemu dada yangu baada ya kufariki 2022 tuligawana watoto sisi ndugu zake, hili tukio limefanya nimkumbuke marehemu dada yangu aliye fariki Kwa maumivu makubwa ya kansa akiwa mikononi mwangu, nawaza Bora kuachana na mke wangu kuliko kuacha mtoto wa dada ateseke ntakuwa nimemkosea dada.

Mke wangu alimchukua mtoto wa kaka yake anaishi hapa na anaelekea kumaliza form 4 Kwa Gharama zangu, ila mtoto wa upande wangu kashindwa kumlea Kwa miaka miwili tu,hii ni sawa kweli?

Halafu baada ya mtoto kuniambia kuwa yeye ndo alimpiga, muda wote saivi ni kumuangalia Kwa jicho Kali sana na kumwambia eti ametumwa aje kutugombanisha, mtoto wa miaka 8 anawezaje kutugombanisha?

Sikuwahi kumfikiria mke wangu kuwa anaweza fanya hiki alicho fanya kutokana na mambo ninayo wafanyia ndugu zake, na ndiyo maana huyu mtoto nilimleta hapa Kwa kuamini atamsimamia kama mwanae na kama anavyo wasimamia watoto wetu wawili.

Mpaka naogopa kwenda kazini na huyu mtoto kumuacha hapa, nahisi atampiga Yani

Da kwa uchungu kabisa pole ndugu yangu ila tatizo linaanzia kwako bila shaka huna kauli katika nyumba yako sio mtu wa kuheshimika na familia yako mungu akutangulie
 
kama unajua mkeo ana tatizo na kukaa na watu,ni simple tu,any ndugu,mtoto wa mtu asie wake,etc usiwalete hapo kwake

watunzie huko huko walipo,au kama vipi wachukulie nyumba ingine pembeni huko

otherwise utaharibu nyumba yako just coz unajua "kukaa" sana na ndugu zako.....

nachojua matakwa ya mkeo ndio ya kwanza,mengine ni socondary,sasa wewe yaelekea unafata unachotaka wewe,she will not agree,na ndoa inakua ngumu kwa viburi vyenu wote wawili

unachoshindwa kujua ni kwamba kiburi cha mkeo ndio cha kwanza kukihudumia,ndugu ni mwishoni no matter ni ndugu close kiasi gani regardless

hao ndugu zako watunzie walipo au walelee nyumba ya mbali...hii mambo ya kuadopt watoto bila consent ya mwanamke mwenye nyumba ndio inaleta shida kiasi hiki mpaka ukaleta uzi hapa,it means imeathiri nyumba yako already

get rid of everybody,bakiza huyo mwanamke na watoto wake na wewe,otherwise unasukumizia huyo mwanamke watu asiowataka,aidha ataondoka utabaki na hao ndugu zako unaoona wa maana kuliko comfortability ya huyo mwanamke

Chagua,lay in or lay down
 
Hili mwanamke la hovyo tu! Unaona jamaa anasema lina mtoto wa kakake yuko karibia anamaliza form four kwa gharama za jamaa! Kwa nini ndugu wa upande wa mwanaume wasikae kwake? Kama ni hivyo basi wakubaliane kuachana na ndugu wa pande zote!
 
Huyo mwanamke pona yake ilikua ni baada tu ya mtoto kufika hospitali hatua inayofata ni kwenda kuchukua Pf3 halafu hio kesi ya jinai unawaachia dawati la jinsia waishughulikie.
Hakuna kitu inauma kama kuona mtoto yatima ananyanyasika na kuteseka ndani ya nyumba yako, halafu mtoto mwenyewe ni mpwa wako tena mdogo wa miaka 8.
Mjomba ni mama, kwa huyo dogo wewe unatikiwa u play part ya mama yake.
 
Hii story!!!
Sidhani,hayo mambo yapo. Mimi yalinikuta kwa mtoto wa dada yangu..(natafuta maisha sehemu ya mbali,sikai nyumbani) alisoma O level kwangu..asubuhi anakwenda shule bila kula chochote(wanaficha mkate/maandazi/kiporo cha wali/kande) ili asipate chochote asubuhi.. kuna siku nikifika,alikuwa amekonda balaa.. nikaanza kujua ni nini.. nikiwa nyumbani anamjazia vyakula mezani.. ni mateso. Nilifanya maamuzi magumu hakika..
 
Mbona hiyo ni jinai. Unatunza mhalifu ndani. Toa taarifa serikali za mitaa, ustawi wa jamii
 
Back
Top Bottom