Mke wangu ananidharau nifanyeje?

Mke wangu ananidharau nifanyeje?

Kwani umesikia mke ni drycleaned kuwa akufulie ngue au make no chief kuwa akupikie... Wanaume tubadilike mitazamo na kusoma alama za nyakati... Sio mbaya mwanamke kukufanyia utakacho ila vingine kama unaweza Fanya mwenyewe tena kwa upendo mkubwa
Kwamba mume awe anajipikia na kujifulia mwenyewe na mkewe yupo tu?!!!
Mume akilazimika kufanya hayo majukumu ya ndani (house chores) lazima familia itayumba sana.
Mume ana majukumu yake ambayo mke hayawezi. Huu usawa unaharibu sana wanawake wajinga!
 
Mwanaume hakuzaliwa kufanya kazi za kipuuzi kama kufua wala aina hizo umelea ujinga.
 
Kwanini unataka sasa hivi ndo aanze kukufanyia hayo yote, wakati ndani ya miaka nane hajawai kuyafanya? Na kama uliweza kufua na kujitengea maji bafuni miuda wote huo sasa hivi umepatwa na nini ushindwe kufanya?
 
Kwani umesikia mke ni drycleaned kuwa akufulie ngue au make no chief kuwa akupikie... Wanaume tubadilike mitazamo na kusoma alama za nyakati... Sio mbaya mwanamke kukufanyia utakacho ila vingine kama unaweza Fanya mwenyewe tena kwa upendo mkubwa
Tena hao wa huko ni wanaume wababe sana hata kama yeye majukumu yake kama Mme hawezi , ila anataka yeye mkewe afanye yote yanayompasa kufanya
 
Habari zenu humu kwenye Jukwaa hili pendwa, mimi nimeoa mke ( Mrangi) na tumefanikiwa kupata watoto wa 3 wote wa kike sasa mke huyu mwaka wa 8 huu hajawahi kuniwekea maji bafuni wala kunufulia nguo zangu sasa watoto wangu hatimae wamekuwa na wameanza kujitambua, kinachoniuma ni kuona watoto wakishuhudia mimi kama baba wa familia nikiwa nafua nguo zangu mwenyewe mke nikimwambia anifulie wakati mwingine anajibu kabisa kuwa sifui hali hii inanishangaza na kunisikitisha sasa naombeni ushauri nioe mwingine au nifanyeje upendo kwake kiukweli haupo kutokana na anavyonidharau naomba ushauri wenu.

Nawasilisha.

Pia soma: Asanteni Jf kwa ushauri wenu na hiki ndicho nilichokiamua
Pole yaani kuanzia siku ya kwanza mpaka miaka 8 ndiyo ukaiona shida? Au ndugu zako wamekushika masikio? Maana watu wa huko Bunda wana mdomo hasa wanawake hata kama yeye ndoa yake imemshinda lakini ya kaka yake ataikomalia huyo, na ulitakiwa uangalie shida inaanzia wapi kama ndugu zako hawakumkubali lazima walete figisu za hapa nà pale, ila kwenu mnaoga ziwani hata mjini unajitengea tu [emoji3] pole sana kilema umekifuga mwenyewe.
 
Hakuna mwanamke mjeuri mbele ya mwanaume mwenye pesa
Pesa ndugu sio kila kitu na kazi uwe unaiweza, sasa lundika pesa zako hapo halafu kazi mbofu mbofu, unamjazia mikuku, misamaki, huku unamshindisha kapa mpaka anafanana na ukuta wa sebuleni lazima hizo pesa akawape wanaoweza kazi, ndoa si pesa hizo ni chachandu tu.
 
Pale mapenzi yalipokuwa ndindi ukajifanya unajali kila kitu acha tuu mke wangu ntafanya...sasa ndo uendelee kufanya..halafu hayo mabafu ya kupelekeana maji ya wapi hayo? Siku hizi anakuta maji humo humo achague mwenyewe hot or cold.
 
Pesa ndugu sio kila kitu na kazi uwe unaiweza, sasa lundika pesa zako hapo halafu kazi mbofu mbofu, unamjazia mikuku, misamaki, huku unamshindisha kapa mpaka anafanana na ukuta wa sebuleni lazima hizo pesa akawape wanaoweza kazi, ndoa si pesa hizo ni chachandu tu.
Hahaha..
Lazima ajue kumtoa maji, eeh😁
 
Dawa ya mwanamke no mwanamke mwenzake.
Tafuta mwanamke mwingine ukaoe acha kuzembea bana.
 
Pesa ndugu sio kila kitu na kazi uwe unaiweza, sasa lundika pesa zako hapo halafu kazi mbofu mbofu, unamjazia mikuku, misamaki, huku unamshindisha kapa mpaka anafanana na ukuta wa sebuleni lazima hizo pesa akawape wanaoweza kazi, ndoa si pesa hizo ni chachandu tu.
Ukiwa na pesa hata akikusaliti atakuheshimu ili usimuache ajafa njaa
Pia hata akikuzingua unamuacha unadaka mwingine fasta,njoo kwa masikini basi kama huna oesa utadharauriwa hata na watoto wako mwenyewe
 
Habari zenu humu kwenye Jukwaa hili pendwa, mimi nimeoa mke ( Mrangi) na tumefanikiwa kupata watoto wa 3 wote wa kike sasa mke huyu mwaka wa 8 huu hajawahi kuniwekea maji bafuni wala kunufulia nguo zangu sasa watoto wangu hatimae wamekuwa na wameanza kujitambua, kinachoniuma ni kuona watoto wakishuhudia mimi kama baba wa familia nikiwa nafua nguo zangu mwenyewe mke nikimwambia anifulie wakati mwingine anajibu kabisa kuwa sifui hali hii inanishangaza na kunisikitisha sasa naombeni ushauri nioe mwingine au nifanyeje upendo kwake kiukweli haupo kutokana na anavyonidharau naomba ushauri wenu.

Nawasilisha.

Pia soma: Asanteni Jf kwa ushauri wenu na hiki ndicho nilichokiamua
Swali ulianzaje kufua?
 
We jamaa si bure una wazimu kabisa,

Yan unamuacha mke kwa kuwa hakuwekei maji ya kuoga?? Kama anachepuka ntakusupport umuache ila kama sababu ndio hiyo kaa na mke wako

Kwahiyo unavyoondoka huko unapoenda ndio utawekewa maji ya kuoga?????

Think twice

Hiyo sio sababu ya kumuacha mke

Labda kama hukumuoa na umemchoka hapo unaweza kuondoka
 
Kwanini unataka sasa hivi ndo aanze kukufanyia hayo yote, wakati ndani ya miaka nane hajawai kuyafanya? Na kama uliweza kufua na kujitengea maji bafuni miuda wote huo sasa hivi umepatwa na nini ushindwe kufanya?
D
Swali ulianzaje kufua?

We jamaa si bure una wazimu kabisa,

Yan unamuacha mke kwa kuwa hakuwekei maji ya kuoga?? Kama anachepuka ntakusupport umuache ila kama sababu ndio hiyo kaa na mke wako

Kwahiyo unavyoondoka huko unapoenda ndio utawekewa maji ya kuoga?????

Think twice

Hiyo sio sababu ya kumuacha mke

Labda kama hukumuoa na umemchoka hapo unaweza kuondoka
Mkuu nilielezea kwa kifupi na kuchepuka pia alikuwa anachepuka
 
Dharau haiwezi kuanza tu hivi hivi, tena kwa miaka yote hiyo! Kuna mahali haufiti kama mume. Katika hili, wewe ndio mwenye marking scheme, hivyo jisahihishe.
 
Back
Top Bottom