Mke wangu ananiletea Usuperstar

Kinachonishangaza huyu jamaa, kama alitaka mwanamke msomi kwanini asingeenda kuchumbia mwanamke ambaye tayari ni msomi kuliko kwenda kuokota lingumbaru na kujipa kazi ya kulisomesha wakati Lina wazazi? Mbona wapo mabinti kibao tu ambao ni wasomi na wanahitaji kuolewa!?

Hii tabia ya ku-take advantage kwa kusolve matatizo ya mtu ambaye yuko disadvantaged muda mwingine naona imekaa kionevu sana na ni ya kishenzi na dunia Huwa inawapa malipo stahiki yao watu wa dizaini hii.
 
Duh! Mkuu pole sana.

Ulimsomesha level gani?
 
[emoji16]
 
Hiyo ndo Hali halisi
🤣🤣
Hata tukikaza ni Ile hatutaki kuonyesha
 
Bandiko lako limejaa madini sana ndugu na ndio sululisho la yanayoendelea kwenye taasisi ya ndoa.

Ila kwa bahati mbaya hii version ya mwanaume uliyoielezea kama ndio mwarobaini wa changamoto zote wanaume tunazopotia kwenye ndoa inapigwa vita sana na jamii.

Mwanaume yeyote yule anayeishi kwa kuafuata pillars za mfumo dume ni adui mkubwa kwenye jamii, jamii yetu ya kileo mwanaume kama huyo inamuita toxic man na tayari imesha mredefine mwanaume halisi yukoje.

Na huyo mwanaume jamii ambaye jamii inampigia chapuo ndio huyo ambaye wanawake mna msumbua sana. Kwa ufupi jamaa ya kileo inampa promo mwanaume dhaifu.

Na hata nyie wanawake wa kileo tayari mmeshafundishwa kujihami dhidi ya mwanaume anayeishi kizamani, hivyo ni vigumu sana kuishi kama mababu zetu katika jamii hii ambayo tayari imeuangusha mfumo wa maisha walioishi mababu zetu, ni sawa na wewe mkristu kuishi kwenye mji uliojaa waislamu halafu unataka uwe unakula kitimoto kila siku, utakula sawa lakini kwa tabu sana na hautakuwa comfortable.
 
Kuna mtu anakuja huko
 
Duh[emoji22]
Sipendi Mimi haya mambo
Sijui tuna shida gani wanawake [emoji119]
Mpotezee Kwa muda,usiombe unyumba kabisa,piga kimya!
Mwanamke wa hivyo ukimpotezea kumuomba unadhani atashtuka? Ilishawahi kunikuta hiyo,nilipotezea mpk ikafika mahali nikapoteza hisia na yeye kabisa hata avue nguo zote mbele yangu hata sishtuki.
Akaanza kulalamika yeye sasa hapo ishapita miezi sita (6) tunalala tu kama dada na kaka.
Ikafika mahali akawa anataka yeye mimi mood ilishakata tena hata afanye nini mawazo yangu hayapo.
Akaanza kulalamika kuwa eeeh wameshakuloga huko nje [emoji22] nikawa naishia kutabasamu tu.
Vikaendelea vingi mpk ikafika mahali nikaaga mashindano nikaanza maisha yangu mengine.
Ukishasaidia watu wa namna hii umejipalia makaa kichwani Jiandae.
 
Boss Pole kwa yaliyokupata,hii hali ya kusahau walikotoka huwa inawakuta Wanawake wengi ambao waliokotwa kutoka ktk hali ngumu ya kimaisha,wanapopata mafanikio Kidogo tu,basi huanza majivuno na,dharau kwa watu na kwa wale waliowawezesha.Mimi imewahi kunitokea nilimsaidia ndugu yangu wa kike lkn Matokeo yake hadi leo hakuna mawasiliano,Nina jamaa zangu wengi yamewakuta pia.Wewe shukuru amekuzalia hata Watoto.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Pole sana mkuu
 
Hivi mleta mada ni mgeni hapa jf? Mwanamke hasomeshwi! Ukimsomesha fanya kana kwamba umemsaidia kama sadaka! Unapomsomesha mtu unampa uwezo wa kujitambua na pia uwezo wa kiuchumi na kama mtu hajielewi ni rahisi kusahau alikotoka! Watu wanasahau wazazi sembuse wewe?
 
Upo sahihi! Maana ya kuishi na nyie kiakili ni pamoja na kuwa na ustahimilivu. Ni kujua kuwa hata mwanamke anapotoka. Kuwa na uvumilivu (akili) katika ndoa ni jambo la muhimu. Akipanda wewe jishushe kiakili, nakuapia kuishi na mwanamke ni kazi. Mascout hunena ‘be prepared’, kuishi na mwanamke kunatakiwa kuwa na tathimini ya haraka kwa kila jambo analolifanya au neno analosema. Ukiona kuna hatari mbele, Jaribu kuizuia mapema ili isilete matatizo mbeleni. Ukiona dalili za kutokuheshimu jua kuna kidume kinammendea au kimeonja; kidhibiti mapema. Uzuri wa wanawake kama bado anakupenda, atasitisha! Ukibweteka akazoea, ameondoka huyo. Ila Baadae atajuta kwa uamuzi wake, which will be too late.

Sie tupo nao mwaka wa 36 lakini hakuna rangi hatujaona. Pamoja na uzee bado tunaishi nao kwa akili.

Piga ua ndiyo marafiki zetu wakubwa, pamoja na mizengwe yote.

Kwa ambao hawajaoa, oa mwanamke ambaye anaona fahari kuolewa nawe, si yule unayeona fahari kumuoa.
 
Amekuzalia watoto wangapi? Kama ni zaidi ya wawili ndo malipo yako mshukuru Mungu! Wengine wanafanya drama hata kuzaa hazai! Akijitahidi kamoja! Mxiuuuh! Unakuwa umepigwa mara mbili!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…