Mke wangu anapenda kuwasiliana na Ex wake

Mke wangu anapenda kuwasiliana na Ex wake

Habari zenu Ndugu zangu,jamaa na marafiki zangu.

Hoja iko hivi, nina mke ambaye nimedumu naye kwa mwaka karibu wa 10 na Mungu kanijalia watoto kadhaa.
Ki ukweli tunaishi vizuri mno.ni mnyenyekevu,msafi na ni mzuri mno.
Ila miaka miwili tu baada ya kumuoa nilibaini namba moja ambayo alikuwa haja isave ila ilikuwa ndiyo namba ambayo ilikuwa imepigwa mara nyingi sana.
Nilimbana mpaka akaja akakiri kuwa huyo ndiye aliyekuwa Ex boy friend wake.
Kidume nikampiga marufuku lakini ameendelea kuwasiliana naye mpaka mwezi uliopita Licha ya kufikisha mpaka kwa wazee mara kadhaa kwa sababu hiyo.
Sasa najua kuna wataalamu wa mambo ya mahusiano humu ambao mnaweza kunisaidia nifanyaje kwa sababu ki ukweli naelekea kuachana naye kwa sasa
Hapo mnashea.
 
So sad jamani, kaa nae chini mueleze jinsi unavyoumia sababu ya Huyo ex wake

Huu ni udhaifu wa mwisho kabisa uliowahi kutokea. Ukimjadili huyo X wake inaonesha unam mind. Kwa kuwa unampenda mkeo, tena ni mzuri kwako, tumia utaalam ule ule ulioutumia mwanzo hadi akakuambia uhusiano wao.
Sasa, mpime ujue nia yake ni nini?? Wanawake wana tatizo kidogo. Hupenda kuwahurumia wengine zaidi. Je, jamaa ana mke? Itisha kikao cha wazee umwite umwonye kuwa anachokifanya kitaishia kubaya. Kama vip, mkabidhi aende naye kwake
 
Kama angekuwa hafanyi chochote ya nini kung'ang'ania mawasiliano ambayo yameleta sintofahamu mara kadhaa kwenye ndoa
Tangu uanze kufuatilia, umeshawahi kugundua kitu kibaya katika mienendo yao? Umeshawahi kuona text wakizungumzia mambo wanayofanya?
 
Kuna dem wa mshikaji nampiga miti miaka 10 sasa. Sijui utakuwa wewe ndo mumewe
 
Huu ni udhaifu wa mwisho kabisa uliowahi kutokea. Ukimjadili huyo X wake inaonesha unam mind. Kwa kuwa unampenda mkeo, tena ni mzuri kwako, tumia utaalam ule ule ulioutumia mwanzo hadi akakuambia uhusiano wao.
Sasa, mpime ujue nia yake ni nini?? Wanawake wana tatizo kidogo. Hupenda kuwahurumia wengine zaidi. Je, jamaa ana mke? Itisha kikao cha wazee umwite umwonye kuwa anachokifanya kitaishia kubaya. Kama vip, mkabidhi aende naye kwake
Great idea mangatara
 
Tangu uanze kufuatilia, umeshawahi kugundua kitu kibaya katika mienendo yao? Umeshawahi kuona text wakizungumzia mambo wanayofanya?
Hilo sijawahi shuhudia kwa kweli.ila nimegundua uongo mwingi katika maswali ninayomuuliza mke wangu juu ya huyo ex wake
 
Back
Top Bottom