Pole sana.
Mwanamke akiwa na mimba kuna mabadiliko mengi ambayo hutokea mwilini mwake. Mojawapo ya mabadiliko hayo ni kuwa na kichefuchefu na kutapika.
Mwanamke kutapika (emesis) wakati wa ujauzito ni kawaida na huonekana sana mimba ikiwa changa, yaani kuanzia wiki 0 mpaka wiki ya 12 ndipo inapungua au kuisha kabisa.
Hata hivyo hali hii ya kutapika (emesis) inapokuwa kuwa kali sana kiasi kwamba mwanamke hutapika chochote anachoingiza kinywani huitwa Hyperemesis Gravidarum na huambatana na dalili kama kichwa kutuma, kizunguzungu, uchovu, moyo kwenda mbio nk.
Ukali au viwango vya Hyperemesis Gravidarum hutofautiana toka mwanamke mmoja hadi mwingine na mimba moja hadi nyingine.
Kama mwanamke ana Hyperemesis Gravidarum basi cha kwanza ni kumhakikishia kwamba hiyo hali itaisha na kwa wale ambao hutapika chochote anachokula ni lazima aende hospitali alazwe ili atibiwe mpaka kutapika itakapopungua au kuisha. Hyperemesis Gravidarum hupungua na kuisha yenyewe kadri mimba inavyokua.
Kwa hiyo mpeleke hospitalini akapatiwe matibabu mpaka atakapoweza kula au kutapika itakapopungua kabisa.
Kila la kheri.