Mke wangu habebeki...

Jaribu kumnyima hela mwezi mmoja uone reaction yake itakuwaje!
 
embu kata huduma ya kutuma hela, sema umepigwa panga la punguzo la kazi. Kwa hiyo huna hela ya kuishi na kama vipi akutumie paund chache kwa mwezi, hapo utajua Muabudu hela na muabudu penzi.
 
Jaman me nataman kumpata mke mwenye IQ ndogo kama huyo,naamini atarekebishika tu make me mwenyewe nishachanganyikiwa kitambo!
 
Kweni mnajenga? Kwa matumiza ya chakula cha nyumbani tu bila ada yeye na mwanae ni more than enough! Hiyo hela atakuwa anamhonga mtu, haki ya nani vile!
 
ndoa hizi bana, zina mambo.... watu tunatamani kuingia humo kumbe ndani kwafuka moshi!!!!
 
yuko kimaslahi achana nae. Hata angekuwa anakaa london na mwanaye 1000us inatosha. Labda anajenga kwao timua huyo mnyonyaji
 

Kakangu kama hiyo story ni kweli, i feel unavyopata uchungu, huyo mwanamke ni mpumbavu kuliko wanawake wote.

Nakuomba kaa ujifikirie mara mbili, huyo mwanamke siyo kabisa. Najua maisha ya ughaibuni yalivyo, yeye ni limbukeni na anawashauri wabaya nahisi, watu wengi ambao hawajafika ama kuishi ulaya na marekani huwa wanadhani huko kunahela za bure za kuokota tu, kumbe hela ni ngumu kuliko bongo.

Kama yeye anafanya kazi hata ungemtumia dala 500 bado ni nyingi sana.
 

Funga safari mchukue mtoto muweke na mama yako mzazi (ikiwezekana). Kama mtoto ni mkubwa mweke boarding. Kikubwa kabla ya kumtema fikiria namna ya kuangalia mwanao hatima yake ni nini. Hapa unapigana vita na watu waliojificha nyuma ya mkeo. You do have a virtual war pressured by peer group mkuu. Some thing is very wrong with your family and something must happen too, fanya maamuzi magumu majibu unaendele kuyapata hapa hapa JF. Heko JF
 

Jamani wewe usinichekeshe yaani kuna mtu anashindwa kutoa mchanganuo!? Hiyo sio solution hata kidogo, nakawambia anaweza kuleta mchanganuo hadi akaona na hela anazomtumia ni cha mtoto. Bwana kama alivyosema mchangiaji mmoja kwamba apigwe deshi mwezi mmoja au hata miwili kabisa tuone atafanyanini, nakwambia baada ya hapo hata akiletewa $ 500 atashukuru...

Yaani wanawake wengine bwana sijui vipi, kuna wenzao waume zao wako hapa hapa hawaachiwi hata senti tano, yeye mume wake yuko mbali anamkumbuka halafu analeta useless poses, ameniudhi kweli...
 

Malezi ya wazazi kwa watoto ni muhimu lol, asipelekwe boarding wala nini, tusiige tu vitu, unakuja kushangaa mtoto akiwa mtu mzima anakuwa mkatili, kumbe hakupata mapenzi ya wazazi toka mdogo, tuache bahati mbaya kama uyatima ndio ulete hizi habari. Huyo baba amshikishe tu adabu huyo mke wake kwa kutomtumia pesa japo 2 months, nina uhakika atasurvive kwa sababu ana akiba ya kutosha mwaka mzima..
 
kaka, ujue ndoa ni kushibana yaani tendo lile la ndoa ni la msingi sana. unaweza usimpe hata hela bado ile hela kidogo anayopata yeye akakutumia tena wewe. unaweza mpa gari na kila kitu lakini bado hayuko sambamba na wewe. hivyo inaonekana wazi kwamba kuna mtu anayecheza mechi vizuri baada ya wewe kutokuwepo na ndiye pengine hata anayekula pesa yako. Ushauri wangu, jaribu kumbwambia aje huko akutembelee huko likizo fulani kama inawezekana halafu muone atasemaje. Akikataa hitimisha kwamba kuna sub akikubali fanya uchunguzi wa kina wakati uko nae huko na baada ya yeye kurudi huku. Halafu utaujua ukweli. POLE SANA MWANAUME MWENZANGU
 
heri ajenge nyumba hata kwao kuliko ukute kuna kibuzi kingine ndo kinachotumia hiyo mihela yote. Mkuu hapo sio bure hadi anakuforce, kuna namna
 
mmmmh hi thread ina uwalikini hivi kwa maisha yetu bongo milioni moja unafanyia nini hata kama foleni ya dar?Tufanye count down ndogo,petrol 300,000 sokoni 120,000 housemaid 100,000,miscelleneous 200,000 laki nane roughly sasa huyo milioni 2 tena ana mshahara?either anajenga kwao au ana mwanaume tena miundombinu almaarufu marioo.halafu kumbe nie wanaume mnajua kuna umuhimu wa kuangalia kabilae?ushauri embu acha kumtumia matumizi mwezi mmja mweleze chochote either umelipa ada or whatever uone reaction yake hata kama uko mbali hisia zitakugusa.pole all the best.
 

Unajua bei ya kiatu CL, ni $ 1000+, pochi ya LV, sijataja nguo na vipodozi kwa mwezi inaweza kuwa $ 1000 pia. Mnaishi dunia gani ndugu.

Ukiwa nacho tumia, ukikosa jutia...... na mkumbuke kuwa landcruser mkonga hainunuliwi show room/yard, hadi kwa order.
 
kama kiatu ni dollar 1000 sio kwao kwa sababu mume wake amesema ndo anayomtumia kwa hiyo unataka kusema ye amenunua kiatu tubila kufanya mengineyo?thread ya mtoa mada sio wa class hiyo na majibu yangu yalimlenga yeye hayakukulenga wewe na matajiri wengine wenye kununua kiau cha milioni na laki sita
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…