Mke wangu hataki- nishaurini

MLUGU

Member
Joined
Aug 12, 2010
Posts
9
Reaction score
0
Baada ya kusikia kuhusu Jamii Forums, nimeamua kujiunga maana nasikia kuna vitu vingi ikiwemo ushauri mbalimbali.

Basi leo naombeni mniksribishe kwa kunipa ushauri kuhusu hili maana linanisumbua na sijui la kufanya. kuwa ni udanganyifu, kawaida au upendo kwisha.

Mimi ni mwanaume niliyeoa na tuna mtoto mmoja wa mwaka 1 na nusu.
Mke wangu ana umri wa miaka 26 nami 32.
Huwa mara nyingi nahitaji sana kuwajibika kindoa, at least mara moja kwa hata siku mbili.
Lakini mwenzangu hiyo mara moja tu kwa usiku anakuwa anasema amechoka tusiendelee,

Kutokana na hilo najicondition ili nisihitaji sana. lakini inapokuja yeye siku hiyo kapenda nitafanya kila niwezalo adi yeye aridhike.
baada ya hapo kupata habari hiyo tabu.
Labda baada ya wiki au 2. kitu ambacho kinanifanya kila siku nihitaji tu kama almasi.

Sasa sielewi huwa hafurahii, au anadanganya au hanipendi, au ninini, Nisaidieni wakubwa
wenye uzoefu.
 
Ndugu yangu kwanza karibu JF, pili pole ya kwa yanayokusibu ila je mkeo anafanya kazi gani? anatoka kazini saa ngapi? na je anasoma shule ya kujiendeleza akiwa kazini? mtoto wenu ana umri gani? kabla ya kuzaa mlikuwa mnafanya tendo la ndoa na kuridhishana? ukinijibu hayo nitakushauri mkuu kwa upande wangu.
 


ndugu yangu uko kama mimi ila mi nazidi kumwambia na kumwombea naona soln ni kati yetu wawili tu akuna atakaetusaidia same to you mwombee usikate tamaa afadhali we umefikisha mwaka na nusu mi ana miezi 7 loh maamini mungu atatupigania kwa hili usito nje ya ndani ni ngumu kuacha mungu akubariki nitazidi kukuombea ama tyuzidi kuombeana
 
dogo ..skia wewe..unataka kila siku hiyo umeambiwa chai?...hujui hata vitabu vikuu vinatushauri "peaneni kwa nafasi"...na umesahau pia "mme hana mamlaka juu ya mwili wake isipokuwa mkewe naye mke hana mamlaka juu ya mwili wake isipokuwa mmewe"?...

pia unatakiwa ujue kuwa wife naye ni mwanadamu pia anakuwa na hisia za mambo mengine zaidi ya tendo la ndoa...pia unatakiwa kujua mbinu mbadala za kum-hamasisha mama atamani kufanya tendo hata kama alikuwa hajisikii.."tongoza hisia za mkeo..seduce her"..... kingine kama mdau alivyosema mama naye anaweza kuwa anachoshwa na mihangaiko ya ki-maisha ...

pia na wewe ukipewa kazi ya kupasua maini unaweza au just unacheza?...usijekuwa unamtia shombo bure hata hamu tena hana...anyway..tafakari....chukua hatua
 
Yaonekana umesha hamaki na kwa kiasi fulani una kasi sana ya kutaka kutuliza kiu yako............hii ni hatari; kwanza tafuta namana ya kushusha huo munkari na hamasa ya ngono kwa kujikeep busy na mambo mengine ..............yapo mambo mengi tu unaweza fanya. Acha kabisa kukumbushia ma kudai ngono! kwa sasa;

Jitahidi sana uishi maisha ya kawida na sio ukbaki ukihesabu when was the last day; onyesha kumfurahia.........ndio kiapoa cha ndoa; I was in the same situation na hapa yes
 
why all married people wana complain sana.????????
 
mwanaume unatakiwa kujifunza
namna ya kumshawishi mwenzio kwa vitendo....

sio kumsumbua kwa maneno kuwa nataka sex....
jaribu kuwa more romantic kidogo....
 
why all married people wana complain sana.????????

It's time tusikie hata good sides za marriage na sie kufarijika!..
Pole kaka mwenye matatizo ila sex 4 times kwa mwezi ni siyo mbaya!!
 
Pole sana mzee, lakini ndo hali ya maisha. Lakini napenda kukuuliza swali kuwa ulishawahi kuongea nae katika suala zima la unyumba? Sidhani kama humrizishi kwani hata huyo child msingempata. Pengine unamuumiza sana mzee wakati wa tendo lenyewe, sabu wanaume wengine mashine zenu noma, hata changudoa anaweza kurudisha pesa ili aondokane na adha.
 
pole sana mdau!kama zamani alikuwa anakupa vizuri siku hizi anakubania basi kuna mambo mawili.....huenda akawa amepata jamaa nje anampa penzi tamu kuliko lako......au ameanza dharau....hii inatokea kwa wanawake hata wanaume haswa kama amepata kazi nzuri au anaongeza elimu!

halafu ukitembea nje ya ndoa ataanza kulia!
plz mweke kitako,itasaidia!
wenzake wanatafuta wanaume kwa gharama yeyote yeye analeta mapozi.....shaurile!
 
Asee, kumbuka kuwa wanawake wanapokuwa na watoto wadogo attention yao huhamia zaidi kwa watoto na ndo wakati wanaume wengi hutoka nje ya ndoa kwa kisingizio cha kutopendwa! Je umeishamwambia ukweli mwenzako kuwa wewe unataka kila siku? halafu hutakiwi kuchoka endelea kumkumbusha pia wajibu wake kwako. Hicho ni kipindi kiumu sana kwa wanaume. Ndo maana wengine huwa hawataki kulala na mtoto kitanda kimoja, hiyo inasaidia angalau mkeo kukumbuka kuwa anamme. Nunua kitanda cha mtoto na awe analala chumbani kwenu lakini kwenye kitanda chake!
 
iwapo hajakupa sababu kuhisi kama 'unamegewa'... jipange upya na uvunje ukimya(kwa hisani ya watu wa JF), itakupa kwa kuanzia.... tafuteni siku(hasa wkend) ambayo utamtia hamasa ya kula tunda(kwa simu, kwa sms) na akiridhia msifanyie hapo, hameni muende hata hotelini... huko jipe nafasi ya kuvumbua vionjovipya vya mapenzi yenu... HEBU CHAKARIKA KIDOG KIJANA, USITUTIE AIBU NDUGUZO...ebo?!!!!:glasses-nerdy:
 
Kwa umri wa mtoto huo, yawezekana inachangia tatizo. Je mke anapumzika vya kutosha au anafanya kazi tena ngumu za ki-tysone tysone? Mwanamke akiwa amechoka ashiki yake kimapenzi hushuka, tena nisene hasi kabisa. Je ndani kuna upendo wa kutosha au ni amri tu na hakuna kutaniana taniana? Lugha yako kwa mwenzako ni silaha tosha. Usitegemee wewe utakuwa mume naggying au mropokaji maneno ya kuchefua kwa mkeo halafu eti utegemee mapenzi toka kwake. Women are delicate creatures! Hebu eleza kwa uwazi mnavyoishi na huyu mke wako ndipo tutaweza kukupa ushauri hapa.
 
Tumzungumze yanayotuhusu ili tulinde mahusiano yetu eeeh (Tangazo ili limekujia kwa hisani ya watu wa Marekani) sikiliza vizuri yale matangazo kuhusu samaki Sangara, familia inayoandaa kuku na mengine ujiweke kwenye kundi husika. Hawa jamaa wamekuja na mradi mzuri sana hapa nchini tulikuwa tunafurahia miradi ya malaria tu na UKIMWI wakati mahusiano ni mabovu ndoa zinavunjika na kusababisha yatima na wanandoa kutoka nje na kupata maambukizi ni bora kuboresha upendo ndani

Ushauri:
Masuala ya unyumba yanaleta shida sana kwenye mahusiano kama hamna mawasiliano mazuri. Jaribuni kuongea na kuandaana mapema sio mnakurupukia tu kitandani jenga mazingira ya unyumba toka mchana, kama mkijikuta mko wawili mchana jaribu kumkumbatia na kumbusu, siku unamlisha nyama kwa mdomo kwa mdomo kama ile style ya keki ya harusi, unamletea vijizawadi kama chupi na kumwomba ajaribu mbele yako, kuoga pamoja kula chakula sahani moja, kutoka out pamoja (si mpk harusi tu) na kuongelea suala zima la kupeana uroda kwa pamoja

Mazingira hayo niliyoyataja yanamfanya mtu atamani ngono na pia kufurahia maisha ya ndoa na kubwa kabisa jengeni mazingira ya utani na urafiki, yana raha yake sio amri kila siku

Pole sana kwa tatizo linalokusibu ila ni la kisaikolojia zaidi jaribu kuliweka sawa mambo yataenda vizuri
 
why all married people wana complain sana.????????

Tena wanacomplain kwenye hilo suala la "faragha". Yatukatisha tamaa wengine humu.

Pole kaka kwa matatizo which in actual sense sidhani kama ni tatizo kihivyo. ongea naye ujue tatizo liko wapi
 
Tena wanacomplain kwenye hilo suala la "faragha". Yatukatisha tamaa wengine humu.

Pole kaka kwa matatizo which in actual sense sidhani kama ni tatizo kihivyo. ongea naye ujue tatizo liko wapi
ilo ni bonge la tatizo fikiria mtu dudu limesimama mkewe yuko naked kalala jamaa anamtamani lakini unyumba hapewi nakwambia unaweza kurukwa na akili na hiyo inatokea daily mpk upewe wiki 2 zimepita unadhani huyo mtu ataweza kuconcentrate kazini kweli?
 


Lakini kweli aisee ni tatizo kubwa. Bora umenijuza zaidi FD
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…