Mke wangu kabeba mimba 3 mfululizo; kiafya haitamdhuru?

Mke wangu kabeba mimba 3 mfululizo; kiafya haitamdhuru?

NGARUKA

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2014
Posts
401
Reaction score
70
Habari zenu wana JF?

Aisee kuna vitu binadamu inabidi tumwachie Mwenyezi Mungu tu jamani.

Niliooana na mke wangu 2013 na mwaka huo huo Septemba mimba ikatoka ya miezi mitano mtoto wa kiume. Tukaaa kidogo ikaingia ikatoka nyingine Mei 2014. Baada ya hapo ikaingia tena ikatoka Agosti 2015.

Sasa maajabu wengi walianza kusema "ooh mkeo kizazi kimelegea". Tukatembea hospitali nyingi hapa Mwanza wakawa wanasema ikitokea amebeba mimba nimpe total bed rest. Madawa ya kienyeji nayo hatakuwa nyuma alikunywa sana.

Sasa 2016 akajifungua mtoto wa kwanza, haraka haraka 2017 Oktoba akajifungua tena mtoto mwingine. Yule dogo akiwa bado anatambaa ameshika tena mimba[emoji134][emoji134][emoji134].

Yaani mimi namhurumia sana mke wangu ila nahisi yeye anapenda hii hali. Hata michepuko kanizuia kabisa hasira zote zinaishia kwake.

KIAFYA INAKUWAJE KWAKE?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata wewe ni chanzo cha tatizo.
Mnashindwa hata kutumia njia local za kupanga uzazi? Hata kalenda inawashinda?
Au unataka watoto wote wawe mafundi viatu?

kuanzia leo ieleweke kwamba "Tecno sio Simu"
 
Mkuu hongera, hii tiba mmepata wapi ili na wengine wenye mahangaiko kama hayo wakapate tiba.
 
Tatizo ni lenu wote wewe unajua kudandia tu haujui side effects hata kujizuia siku ngapi ngapi mnashindwa jifunzeni kujizuia ila sikussikushauri vidonge vya uzazi hakuna maana hakuna ambazo halizina madhara
 
mnabebeshana tu mimba kama simbilisi vile
 
Huyo mkeo hana ndugu aise? Unatakiwa ukamatwe upelekwe DAWATI, huo ni ukatili.
 
Si akaweke kitanzi cjui hahaaaa maisha yalivo mtaweza kuwalea kweli? Punguzeni speed mkeo hajihurumii

Sent using Jamii Forums mobile app
Maisha Yana shida gani?
Watoto wanakula kilo ngapi?
Shule bure
Nguo mtumba elfu moja moja..

Unawapa kilichopo,

[emoji252] [emoji479]
 
Maisha Yana shida gani?
Watoto wanakula kilo ngapi?
Shule bure
Nguo mtumba elfu moja moja..

Unawapa kilichopo,

[emoji252] [emoji479]
Kwa mfulilizo wa huyo Dada 2016,2017 sasa hao watoto kuwatunza ni rahisi hivo, hata ka hawali kilo ngapi maisha yetu Watanzania yanajulikana bwana sikuhizi ni tofauti na enzi za baba zetu aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mfulilizo wa huyo Dada 2016,2017 sasa hao watoto kuwatunza ni rahisi hivo, hata ka hawali kilo ngapi maisha yetu Watanzania yanajulikana bwana sikuhizi ni tofauti na enzi za baba zetu aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimelea wanangu kwa mfulilizo tena ni rahisi
Wanakuwa na mahitaji yaliyofanana
Kama uji unajua wote wanakunywa uji

Maisha ya jamaa unayajua?

[emoji252] [emoji479]
 
Kiafya kwa upande was mama
1. Anaemia( upungufu wa damu) sababu ni moja mama akishajifungua hanabudi kupata muda wa kurudi katika hali ya awali(pre-pregnancy state) atleat for 1 year and 6 months up to 2 years.
2. Sambamba na hilo inamuweka mama kwenye hatari ya kupata matatizo wakati wa kujifungua ikitokea

Kwa mtoto
1. Inapungua bonding kwani mama hana budi kumuachisha kunyonya mapema
2. Matatizo yanayoendana na kukosa lishe stahiki inayotokana na maziwa ya mama m.f kwashiorkor (due early weaning) na kadha wa kadha
 
Habari zenu wana JF?

Aisee kuna vitu binadamu inabidi tumwachie Mwenyezi Mungu tu jamani.

Niliooana na mke wangu 2013 na mwaka huo huo Septemba mimba ikatoka ya miezi mitano mtoto wa kiume. Tukaaa kidogo ikaingia ikatoka nyingine Mei 2014. Baada ya hapo ikaingia tena ikatoka Agosti 2015.

Sasa maajabu wengi walianza kusema "ooh mkeo kizazi kimelegea". Tukatembea hospitali nyingi hapa Mwanza wakawa wanasema ikitokea amebeba mimba nimpe total bed rest. Madawa ya kienyeji nayo hatakuwa nyuma alikunywa sana.

Sasa 2016 akajifungua mtoto wa kwanza, haraka haraka 2017 Oktoba akajifungua tena mtoto mwingine. Yule dogo akiwa bado anatambaa ameshika tena mimba[emoji134][emoji134][emoji134].

Yaani mimi namhurumia sana mke wangu ila nahisi yeye anapenda hii hali. Hata michepuko kanizuia kabisa hasira zote zinaishia kwake.

KIAFYA INAKUWAJE KWAKE?

Sent using Jamii Forums mobile app
Akijifungua hii aanze uzazi wa mpango watoto waliotangulia wanaweza kudumaa lakini hata familia inaweza kuyumba kimapato maana kuwalea watoto watatu wanaofuatana ni ngumu.
 
Lways wanawake waliopata matatizo ya kuchelewa au mimba kutoka toka kama wako, wakifanikiwa paaap huwa hawataki kungojea wanabambikiza mpaka idadi yake itimie maana anaona akisubiria tatizo litajirudia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom