Mke wangu kanificha mengi, naomba ushauri

Mke wangu kanificha mengi, naomba ushauri

Covax

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2021
Posts
10,198
Reaction score
35,323
Ndugu zanguni habari zenu, nimekuja kwa ushauri wenu pamoja nakuweza kupanua mawozo yangu nakupunguza stress za kifamilia.

Mimi nina mke na tumejaliwa watoto wawili (2) wakike na wakiume, Mwaka jana mnamo mwezi wa saba (7) mke wangu alinipa taarifa kwamba Mama wake mzazi (mama mkwe) anakuja mjini nijiadae kwenda kumpokea hiyo siku ikifika na ni sisafiri paka nimpokee, kwasababu shughuri zangu nasafiri za nje ya mkoa, nikamuliza amekuja kufanya nini? Eti kufuatilia mafao yake ya pensheni, mmh wakati alisha pokea tangu mwezi wa pili, niliguna tu nikamjibu sawa ntampokea, baada ya kama siku tatu aliniambia amepanda basi, siku hiyo nikaendesha ki 'babywalker' (gari) changu nikaenda standi ya ma basi ya mikoa kumpokea, alingia kama saa sita usiku nikampokea nikaweka mizigo yake ndani ya gari tukaelekea nyumbani vizuri bila kunotisi kitu chocolate.

Baada kama ya siku mbili mie nikasafiri kuenda kwenye kazi zangu, nilirudi baada ya siku tatu (3) nikamukuta bado yupo si ku mind walaa, sisi kiutamaduni na kimila mama mkwe ni mwiko kwangu kuingia chumbani mwake au kumshika mkononi au kutumia choo kimoja kwahiyo nilikuwa namsalimia nikiwa sembuleni kila asubuhi na jioni hiyo wiki nilio kaa sikumtizama sanaa isipokuwa usiku wakati namleta aliendelea kukaa nyumbani kwa takrbani miezi mitatu, mie naenda safari zangu na rudi kila wiki kwa kufichwa na mke wangu.

Kumbe Mama alikuja kufanikisha masuala mawili: hayo yote nilikuja kugundua badaye sana.

Yule mama alikuja kuugulia kwangu auguzwe na mtoto wake (mke wangu) na kuaga watoto wake wengine walioko jijini. Kwangu ndo pakawa kitovu cha mikutano na kuendesha vikao vyao wakati mimi sijui lolote.

Wife kanificha sijawahi ku-imagine kitendo kama hicho. Kumbe mama alikuwa ameshaathirika siku nyingi na virusi vya huu ugonjwa wa kisasa (VVU). Mwili wote ulikuwa umejaa vidonda na ulishabadilika kuwa mweusi na vipele kote.

Kuna siku nilichelewa kutoka nikakuta watoto wake wote watano wako nje, nikashangaa lakini sikumind sana kwasababu wife kaniambia wamekuja kusalimia mama yao. Nikasema poa kumbe kilikuwa kikao cha familia.

Huyu suala la pili baada ya kupokea pensheni yake alikuja kununulia watoto wake nyumba kama kitega uchumi kwasababu siku zake zilianza kuhesabika, kifo kinasongea na hali yake iliendelea kuzorota.

Lakini kumbuka mtoto wake wa mwisho ana miaka 27. Alifanikiwa kupata nyumba hapa mjini, alivyofanikisha hayo akawa anataka kuaga kurudi mkoani baada ya kukaa kwangu miezi mitatu bila mimi kujua. Hata hakuniaga, natoka safari zangu nakuta mama kasharudi mkoani wife ndo kanipa taarifa eti amenipa salamu tu.

Kama mtafutaji na asiye na makuu wala kinyongo niliyapuuzia wala wife sikumuuliza tena kuhusu Mama. Nilikaa nyumbani kama siku tano hivi, tena nikawa nataka kusafiri kuenda kwenye biashara.

Kama kawaida nilimuachia mahitaji ya nyumbani nikaondoka. Baada ya siku kama mbili wife kanipigia simu huku analia tena kilio chenyewe cha kwikwi. Nikamuuliza kulikoni, kanijibu mama anaumwa kalazwa hospitali ya rufaa na kawekewa oksijeni.

Niliduwaa kwasababu sikuwa na taarifa yoyote nyuma kwamba alikuwa anaumwa. Nikamuuliza alipata ajali? Akajibu hapana nitakuambia we tuma pesa niende nimuone.

Sikuchelewa nilijipigapiga nikamrushia laki mbili za nauli na kujikimu. Alivyofika nikaanza kumuuliza mama anaumwa nini hanijibu. Nilikazana kweli kweli kumuuliza kweli ila anaishia kuniambia yuko kwenye oksijeni.

Nikagoma kumtumia pesa mpaka aniambie Mama anaumwa nini? Baada ya siku mbili kaniambia ila baadhi ya wake zetu ni waongo tena uongo wa kitoto. Aliniambia eti anasumbuliwa na (ulcers) vidonda vya tumbo, ndo kawekwa kwenye mtungi wa oksijeni!!!!!!!

Ilikua Alhamisi mwezi jana mtu tunayefamiana naye ambaye ni jirani na ukweni pale kanipigia simu kunipa pole ya kufiwa.

Sikutaka kumuuliza nani amekufa angejua kama kuna usiri mkubwa kati yangu na wife na angenishangaa kutojua huo msiba. Niliitikia vizuri na nilihisi atakuwa mama ndo amefariki.

Kusema ukweli wife hakunipa taarifa mpaka saa 11 jioni wakati mtu alifariki saa mbili asubuhi. Nilijiongeza haraka nikapata usafiri mpaka mkoani. Nilifika mapema tu kwasababu nilikuwa na hela ya ziada nikapanda ATCL ya mchana nikidhani mazishi yatakuwa siku hiyo hiyo. Wife anakuja kunipa taarifa tayari nimeshafika kwao, hana taarifa, lengo lake lilikua nishindwe kuhudhuria mazishi.

Mazishi yalipangwa kesho yake saa saba. Wife alidhani kuniambia saa 11 sitaweza kupata usafiri wa haraka ili nikae na wafiwa pamoja na nzengo.

Kusema ukweli nilishindwa kukutana na wife hiyo siku kwasababu hasira na jaziba nikakimbia makaburini kule kushiriki na wachimbaji. Kule ndo nilipata mkanda mzima wa kuugua na kufa kwake mama mkwe wangu.

Watu wana maneno wanadai “alikufa kwa ngoma” eti alienda kujificha kwa watoto wake jijini. Anyway nilipata kila kitu pale vyote wife alivyonificha.

Sasa naomba msaada wa ushauri kwenu. Siku 40 (arobaini) zimetimia na dua ya arobaini tayari. Wife tangu wiki jana ananipigia simu nimtumie pesa za kurudi nyumbani. Nilisita kidogo sijamjibu chochote kwa sababu bado nina hasira nae, kunitumia kama boya-jinga-fala kwa kunificha hayo yote.
 
Nahisi mke wako alihisi kwamba akikwambia mama ana hako ka-ugonjwa labda ungemzuia afikie kwako na mengine mengi.. ila cha kukushauri hapo Mkuu we mtumie tu nauli aje nyumban kisha ukae nae vizuri kumuuliza kwanini hakukuweka wazi na pia muonye wakati mwingine asirudie hiyo tabia ya usiri sio nzuri...Hakuna kosa lisilosameheka mkuu...sisi wote sio wakamilifu mkae chini myamalize..
 
Sawa Dada ila kuficha kifo cha mama mzazi its... too big to swallow, ina nipa headache sana kuna kumsamehe ila bado unalo mwoyoni....
 
Sawa Dada ila kuficha kifo cha mama mzazi its... too big to swallow, ina nipa headache sana kuna kumsamehe ila bado unalo mwoyoni....

Hakutaka ujue ugonjwa wa mama yake ndio maana alikuficha msiba.

Nadhani huo ugonjwa wa mama yake aliuchukulia vibaya akahisi nawe pia utamjudge mzazi wake.Muache aje muyazungumze punguza hasira.
 
Mkuu pole sana kwa yalio kufika zote ni changamoto za maisha ukisha zaliwa na kuishi changamoto lazima ziwepo tu, ila kwa ushauri wangu mdogo hembu tuliza hasira kwanza na umtumie nauli arudi nyumbani, hili ni kutokana na yule ni mkeo tu, hivi sasa changamoto tunazo pata wanaume na wake zetu ni nyingi zaidi likiwa swala la uaminifu katika ndoa imekuwa tatizo kubwa mno na lina umiza sana.

kwa niaba ya wanao wawili kama Baba usiwatese waje waishi maisha ya mzazi mmoja koz kwanza una onekana ni mtu mtaratibu, hembu jidai mjinga acha mke arudi nyumbani mwendele kulea wanenu wawili wakue japo ukae na kuliweka akilini mkeo ana usiri mwingi so utaishi nae kwa akili.

Garama za maisha hivi sasa ni kubwa swala la kwenda kuoa tena au kuwa na nyumba mbili ni kitendo cha kuongeza garama bila sababu kuu, ili mradi wewe sio mtu wa kuwa nyumbani mda mrefu ni mtu wa safari jitahidi ufiche chuki na hasira juu ya huyo mke ipo siku utasahau na maisha yatasonga mbele bila kuwa umetoa uamuzi mgumu ambao baadae na siku hadi siku ungezidi kukuongezea garama za kulea familia huku na huku.
 
Mkuu nashukuru sana kwa ushauri maridhawa.....ila changamoto iliopo ni roho yangu kukubaliana na ukweli kwamba nimsamahe, napokumbuka jinsi alivo kua ananiomba pesa ya nyumbani matumizi yaliongezeka maradufu, wakati inaenda kwa matibabu ya kificho kwa mama inauma sanaaa duh.....
 
Hilo nimegusia pia ita kuchukuwa mda kidogo kusahau mkuu ila faida ulio nayo wewe sio mtu wa kwenda kazini na kurudi kila siku huwa una safiri, so katika mihangaiko yako ya kazi uta pata nafasi ya kuwa nae mbali kwa mda huku unaendelea na shughuli zako kama kawaida bila ya wewe kuvuruga au kuachana na familia yako, baada ya miezi kadhaa moyo wako utarudi na maisha yata kuwa sawa mkuu, so wewe tuma nauli akirudi wewe safiri kikazi nenda kaa huko jiliwaze, kama unatabia ya kupiga simu piga kama kawaida siku ukitaka rudi home wewe rudi. baada ya mda mambo yatakuwa sawa mkuu niamini kwa hilo wazungu wanasema "Time Heals" so muda utasema tu jikaze japo inataka moyo kuishi na mtu mwongo.
 
Back
Top Bottom