Mke wangu karudi kwenye dini yake

Joined
May 23, 2023
Posts
65
Reaction score
136
Habari wakuu,

Naombeni mnishauri.

Mimi nilioa miaka 18 iliyopita mpaka niko na mke wangu tuna watoto kadhaa na mali kadhaa. Sasa huyu mke wangu alikuwa mkiristo mimi muislam kwenye kufunga ndoa ni yeye alibadil dini na tukafunga ndoa ya kiislam.

Tumeishi vizuri miaka yote hiyo kwa amani na upendo.

Sasa hivi karibuni nimegundua mke wangu amerudi kwenye dini yake na nimemuuliza amekubali na amesema uislam umemshinda kama nampenda niishi nae hivi hivi tu na ukiristo wake.

Sasa jamani niko njia panda sjui nifanyeje maana naona kama watoto wangu watahangaika mara leo mskitini kesho kanisani.

Hebu nisaidieni.
 
Pole sana mkuu kwa yaliyokukuta.

Kwanza fuatilia vizuri ujue huwenda uisilamu unaruhusu kumuoa asiyekuwa muisilamu, fuatilia hiyo kwa mashekhe wa kila aina utapata jawabu zuri kama inafaa ama haifai.

Ukishajua kwamba inafaa basi jambo la kwanza linalobaki ni ndoa iendelee, kwa sababu miaka 18 sio kidogo na endapo mkiachana italeta shida pengine.

Lakini kuhusu watoto wewe usijali jambo la msingi ni mama asilazimishe awabadili na watoto hapo atakuwa ana kuoutshine na kulazimisha yeye ndio adominate.

Hakikisha watoto wanapata malezi mema kwa sababu hakuna dini inayofundisha maovu.
 
watu wengi hua wanabadili tu dini ili kufunika kombe mwanaharamu apite hapa nazungumzia wanaobadili kwaajili ya ndoa wapo kibao tu hawafurahii watoto wao pia kufuat imani yao mpya ila wengi huendelea kugonga kitimoto na wengine huenda kanisani kisirisiri na wengine wazwaz kama mkeo
 
Unaweza kumbadilisha mtu dini halafu usimfundishe au kuwa kielelezo kwake, kwahiyo mtu anaona bora aendelee kupiga [emoji91][emoji91], mfano unambadilisha halafu wewe mwenyewe hata kwenye nyumba ya ibada hauendi unategemea nini hapo, miaka 18, mingi sana kaeni chini myamalize, mambo yakuachana tena sio mtatesa watoto.
 
Mimi Huwa nasema humu Kila siku,usimumuamini mtu anayebadili dini hata siku Moja.

Hawa watu wanakuwa wanafiki sana. Hasa wanaotoka ukristo kwenda uislamu.

Unabaki kujiuliza; huyu jamaa kabla ya kubadili dini ghafla hivi, alipata saa ngapi muda wa kucalculate gharama za maisha mapya, katika Imani mpya anayoenda kuiishi?

Siku si nyingi utasikia "Barnaba nae amerudi kuwa mkristo baada ya kumuacha aliyekuwa mkewe"... Unafiki mtupu!!!
 
Akirudi maana yake hakuna ndoa imeshavunjika mnaishi sogea tukae kuanzia sasahiv
Ulivombadilisha ulimfundisha uislam?
Wewe unaswali swala tano?
Ulimfundisha kuswali na afuate mafundisho yake?
Ushauri Bora sana huu.

Watu hufanya maamuzi fulani ili kufanikisha mambo fulani. Kwa suala la Imani huyo Mwanamke alikuwa anihitaji ndoa akaipata na ndio maana alikuwa tayari kubadirisha dini ili aipate hiyo ndoa kwa sababu kashaipata na kaizoea anataka kurudi kule uliko moyo wake.
 
Ninaye dadaangu alibadili dini akawa muislamu kisa ndoa.

Akija home anakuwa mkristo na kitimoto anakula, akirudi kwa mumewe swala 5. Siku Moja nilimchana aache huo unafiki anaoufanya, Mungu hapendi huo ujinga.

Mtu akibadili dini, tena kisa mapenzi, kuoa/ kuolewa natemana nae kabisa maana hao watu hawanagana misimamo, kusnitch nje nje.
 
aise pole ndugu!kikubwa angalia heshima yake na utii kwako,mambo ya dini yasiwe kigezo cha kutengana ukizingatia muda mlioishi pamoja,endelea kula mzigo huo shekhe ikiwezekana na mtoto wa kupooza machungu ya kutorokwa kiimani
 
Mwanaume anae ongopa kuacha mke kisa watoto naona kama hana vipaumbele na ni muoga wamaisha, hapo hsmna ndoa mteme maramoja kukuepa madhara hatari ya badaye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…