Mke wangu kipenzi changu rafiki yangu ndugu Dada na mfariji wangu uishi miaka mingi

Mke wangu kipenzi changu rafiki yangu ndugu Dada na mfariji wangu uishi miaka mingi

kiroka

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2018
Posts
358
Reaction score
1,887
Leo ngoja nikusifie mtoto wa kipare, tulianza mahusiano nikiwa chuo mwaka wa mwisho nikiwa chembamba cheusi sivutii nani angenitamani kipindi kile mtoto wa watu kigori cheupe kifupi kinene nilipokutongoza ukanikubalia thax mama be blessed my dear.

Nikapata kazi baada ya chuo tukawa pamoja ingawa mwaka mmoja baada ya kazi nilianza kunawiri mabinti wa pale kazini wakaanza kunitolea macho lkn niliahidi nitakuoa na sikutak kuvunja ahadi yangu kwako japo.

Nikatimuliwa kazi binti wa watu hukuniacha ukanifariji kwa maneno mazito na matamu ukanipa moyo wa kupambana ukasema unaona kitu ndani yangu nakumbuk ulivokua unaniombea wakati kibarua kimeota nyasi barikiwa saana wew binti hakika apatae mke Bora apata kitu chema.

Maisha yakasonga nikawa nasimamia mradi wa mjomba angu mradi ukachanua mjomba akaingiwa na wivu akaanza visa nikataka kumwibia nikaanzishe changu binti wa watu ukanituliza nakumbuka ulinambia acha baraka za kipepo zipite tafuta chako. Nikatoka kwa mjomba mambo yakawa magumu zaidi binti ukanambia giza likizidi alfajiri inakaribia love you so much.

Mambo yakawa magumu zaidi Lakini hukuchoka ulinipa moyo nakumbuk kila biashara tulikua tunafanya ikawa inakufa kila biashara niliotia mkono wangu ilikufa milango yoote ya riziki ilifunga na urembo wako hukudiriki kunisaliti wakati wote ulinambia you will rise again. What a women.

Nakumbuk ilinipiga homa ya miezi 3 mfululizo kila nikipima hamna chochote mke wangu hukunikimbia pamoja na hayo yoote baada ya kupita homa ndio milango ya riziki ikaanza kufunguka mmoja baada ya mwingine thax kwa uvumilivu wako.

Pamoja na kua Mimi ni mwanaume Nina tamaa za kimwili lakini nimechagua tamaa zangu ziwe na limit, nitakueshimu wakat wote, umalaya nikafanya mbali na uso wako na hakuna mwanamke Bora kwangu zaid yako.

Love you again
 
Leo ngoja nikusifie mtoto wa kipare, tulianza mahusiano nikiwa chuo mwaka wa mwisho nikiwa chembamba cheusi sivutii nani angenitamani kipindi kile mtoto wa watu kigori cheupe kifupi kinene nilipokutongoza ukanikubalia thax mama be blessed my dear

Hongera sana mkuu. Vijana wanakatishwa tamaa sana kuwa siku hizi eti mapenzi ya kweli hakuna. Shuhuda kama hizi zinatia matumaini sana. Mabinti wema, wanaojielewa na wenye mapenzi ya kweli wangalipo hata kama ni wachache. Mungu Awabariki na kuwalinda muishi na kuzeeka pamoja mpaka kifo.

Hiyo aya yako ya mwisho kabisa [emoji116][emoji116][emoji116]ina maana gani? Kwamba utafanya umalaya ila kwa kumheshimu huyu malaika utafanyia umalaya wako mbali ili asijue? Kwa nini umfanyie hivi binti mliyetoka wote mbali namna hii?



Screenshot_20220117-202127.jpg
 
Leo ngoja nikusifie mtoto wa kipare, tulianza mahusiano nikiwa chuo mwaka wa mwisho nikiwa chembamba cheusi sivutii nani angenitamani kipindi kile mtoto wa watu kigori cheupe kifupi kinene nilipokutongoza ukanikubalia thax mama be blessed my dear
Hongera
 
Bila shaka umeamua kuchangamsha genge...

Pamoja na kua Mimi ni mwanaume Nina tamaa za kimwili lakini nimechagua tamaa zangu ziwe na limit, nitakueshimu wakat wote, umalaya nikafanya mbali na uso wako na hakuna mwanamke Bora kwangu zaid yako

Mzee baba huyo angelikuwa ni mwanamke bora, usingefanya hizi mambo hapa down...

Thread 'Wivu wa mchepuko unataka kunitoa roho' Wivu wa mchepuko unataka kunitoa roho

Thread 'Sijui Nina matatizo au nipo sawa' Sijui Nina matatizo au nipo sawa

Thread 'Nimevunja ndoa ya mtu moyo wangu safi' Nimevunja ndoa ya mtu moyo wangu safi
 
Hahahaha niliona hizo threads lakini nikajisemea let me be positive

Lakini kwa upande wako naona chai zenye chumvi umegoma kuzinywa hata kama haziku-kill

Hata kama haziku-kill, 😊😊😊
 
Hiyo paragraph ya mwisho mbna kama sijaelewa! Ina mana umeshamsaliti?
 
Bila shaka umeamua kuchangamsha genge...



Mzee baba huyo angelikuwa ni mwanamke bora, usingefanya hizi mambo hapa down...

Th

Thread 'Nimevunja ndoa ya mtu moyo wangu safi' Nimevunja ndoa ya mtu moyo wangu safi
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] licha ya kwamba jamaa kapata what a woman ila yeye anavunja ndoa za watu [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom