Mke wangu na "Mheshimiwa Mbowe!"

Nduka

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2008
Posts
8,553
Reaction score
2,380
Sijakosea jukwaa maana kuna walioanza kununa, mwezenu nyumbani kumeanza kuwa kuchungu baada ya wifi yenu kuanza visa baada ya vikao vya bunge kuanza. Wiki ya kwanza alianza kama utani eti anataka kupendekeza baba kivuli ili awe ananikosoa na kutoa mtazamo mbadala kwa masuala yetu pale nyumbani. Hili nililipinga kwa nguvu zote kwa kuwa sikuwa na uhakika na hadidu za rejea za baba kivuli, wiki iliyofuata akaanza kupinga posho zangu na misafara mikubwa ya marafiki ninapokwenda bar.

Nikidhani itaishia hapo sasa baada kiongozi wa upinzani bungeni kurudisha shangingi lake, yeye sasa ndio amekuja na kali eti anataka kupiga bei ka vitz kake ili tuwe tunapanda gari moja kwenda na kurudi kazini sasa mimi hapo naona kama uhuru wangu unaelekea kunitupa mkono, Nifanyeje wandugu kwa hatua za mwanzo nimepiga marufuku bunge nyumbani kwangu.
 
Ahaaaaa haaaaa nimepinda hiyo mbinu ya shemeji!! Ni wanawake wachache sana wenye uthubutu! Hiyo ndi banamatumizi inayotakiwa duniani! Kaka kuwa kinyonga badilika kulingana na mazingira!
 
Ahaaaaa haaaaa nimepinda hiyo mbinu ya shemeji!! Ni wanawake wachache sana wenye uthubutu! Hiyo ndi banamatumizi inayotakiwa duniani! Kaka kuwa kinyonga badilika kulingana na mazingira!

Tatizo ni huko kubana matumizi kunakoingilia uhuru wangu bana, nilikuwa nitoka kazini napaki pale New Afrika hotel wakati wa Happy Hour sasa hivi hii yote itapeperuka halafu kuna dada jirani nilikuwa namsaidia sana lifti maana yeye ndio kaanza tu kazi sasa wife si atakuwa anambana.
 
Ndio maana mimi nilishtuka mapemaaa. Hamna kutumia gari tofauti kwenda kazini. Haya mambo ya wadada kukusubili kwenye kona uwape lifti marufuku. Tutabana mpaka penati mwaka huu.
 
Maelezo yako yanaonyesha dhahiri ulikuwa humsaidii huyo dada bali alikuwa anakusaidia wewe!Kama hakuna kibaya kt yako na huyo dada why uogope mkeo kupanda kupanda pamoja na huyo dada?
 
Maelezo yako yanaonyesha dhahiri ulikuwa humsaidii huyo dada bali alikuwa anakusaidia wewe!Kama hakuna kibaya kt yako na huyo dada why uogope mkeo kupanda kupanda pamoja na huyo dada?

Mimi ninamsaidia huyu dada kwa moyo mmoja ila kwa kuwa naujua wivu wa kambi yangu rasmi nyumbani naona kama huyu dada atakuja kuchezea vitasa bure.
 
. Haya mambo ya wadada kukusubili kwenye kona uwape lifti marufuku..

Huna huruma na watoto wa wanawake wenzio wewe, asubuhi usafiri taabu unataka mwenzako agombanie daladala na mchuchumio.
 
Ukitaka jua kuwa mkeo mkali hebu jaribu kutoka nae na umpakie huyo rafiki yako...safari haitakuwa ya kazini ila kuwahi hosp.
 
Ukitaka jua kuwa mkeo mkali hebu jaribu kutoka nae na umpakie huyo rafiki yako...safari haitakuwa ya kazini ila kuwahi hosp.

Ndio maana nauheshimu sana mgawanyo wa usafiri katika familia, mambo mengi inaepusha na pia inasaidia kuongeza upendo maana na mafoleni haya ukirudi nyumbani unamuaona wife kila siku mpya sasa mkiwa mnapanda gari moja huwezipata muda wa ku miss
 
Hii ya kuwa na baba kivuli ni dai gumu zaidi kuliko kuuza hiyo vitz !!
 
Huyo mke wako ni Mpinzani typical. Nadhan yupo kwenye mchakato wa wewe kuwa unalala na jeans!
 
safi sana nimeipenda tabia ya dadang,mi cjaona kama ni vibaya lbd kama una vimeo vyako huko njian ndo maana hutaki mtumie gari moja au sehemu ambazo unapitia sio kuzuri unaona kama mkeo atagundua but ina uzuri wake, mwaka huu mtakabwa hadi mtaamua kuoa hizo nyumba ndongo ambazo hamtaki zijulikane
 
Mkuu mie ningekushauri u-act kama M*kinda, endeleza bunge

Hii niliijaribu ghafla nikaitwa kwenye kamati ya maadili

Hii ya kuwa na baba kivuli ni dai gum
u zaidi kuliko kuuza hiyo vitz !!

Ndio maana huu mjadala nikauulia mbali kama kesi ya Lema na Pinda

Huyo mke wako ni Mpinzani typical. Nadhan yupo kwenye mchakato wa wewe kuwa unalala na jeans!

Ikifikia huko na demokrasia yenyewe naitupilia mbali tuishi tu Somalia type

Mimi sina hizo nyumba ndogo ila pia napenda mai aheshimu muda wangu wakuziwahi za baridi pale New Afrika na washikaji, sasa kwenda nae si itakuwa kama naenda na bia baa?
 
Huna lolote amekustukia kwa taarifa ngoja akutia akili ujue kwamba hizo bia ni hela siyo karatasi au unapewa bure. Kaa utulie mtoto wa kiume au hujui mbinu tukufundishe ili mkeo akuamini?

Ni PM nikupe mbinu mbadala1
 
Huna lolote amekustukia kwa taarifa ngoja akutia akili ujue kwamba hizo bia ni hela siyo karatasi au unapewa bure. Kaa utulie mtoto wa kiume au hujui mbinu tukufundishe ili mkeo akuamini?

Ni PM nikupe mbinu mbadala
1

Ndio maana nafanya kazi ili nipate pesa kisha hiyo pesa inistareheshe, itabidi hizo mbinu nizichukue tu maana hii inatoka kwa spicie ile ile.
 
Huna lolote amekustukia kwa taarifa ngoja akutia akili ujue kwamba hizo bia ni hela siyo karatasi au unapewa bure. Kaa utulie mtoto wa kiume au hujui mbinu tukufundishe ili mkeo akuamini?Ni PM nikupe mbinu mbadala1
Naunga hoja mkono.
 
Nilivyoona wifi yenu nimejua kuwa unawalenga wanawake zaidi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…