Nduka
JF-Expert Member
- Dec 3, 2008
- 8,553
- 2,380
Sijakosea jukwaa maana kuna walioanza kununa, mwezenu nyumbani kumeanza kuwa kuchungu baada ya wifi yenu kuanza visa baada ya vikao vya bunge kuanza. Wiki ya kwanza alianza kama utani eti anataka kupendekeza baba kivuli ili awe ananikosoa na kutoa mtazamo mbadala kwa masuala yetu pale nyumbani. Hili nililipinga kwa nguvu zote kwa kuwa sikuwa na uhakika na hadidu za rejea za baba kivuli, wiki iliyofuata akaanza kupinga posho zangu na misafara mikubwa ya marafiki ninapokwenda bar.
Nikidhani itaishia hapo sasa baada kiongozi wa upinzani bungeni kurudisha shangingi lake, yeye sasa ndio amekuja na kali eti anataka kupiga bei ka vitz kake ili tuwe tunapanda gari moja kwenda na kurudi kazini sasa mimi hapo naona kama uhuru wangu unaelekea kunitupa mkono, Nifanyeje wandugu kwa hatua za mwanzo nimepiga marufuku bunge nyumbani kwangu.