Mke wangu

Mke wangu

Zogoo da khama

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2013
Posts
631
Reaction score
592
Mke wangu mimi ni darasa la saba, mimi nimemaliza chuo kikuu ni mhasbu nafanya kazi benki na nina mshahara mkubwa tu. Nilikutana na mke wangu kipindi kaja kuchukua mkopo wa Biashara yake, wakati huo nilikua afisa mikopo. Alinielezea kuhusu Biashara yake, plan zake na namna alivyoanza Biashara nilimuambia ondoka uje kesho. Lakini alipokua anaondoka nilimuita dada mmoja rafiki yangu na kumuambia nitamuoa yule dada, yule ndiyo mke wangu. Hakuamini lakini nilimtongoza nikampata na sasa hivi ni mke wangu.

Ana akili sana huyu mwanamke, kabla ya kumuoa nilikua nisshafanya kazi miaka tisa, nilikua na Gari tena ya mkopo na kiwanja tu. Nilijua sina akili kama yeye hivyo nilimuongezea mtaji kwenye Biashara yake na kumaucha afanye miujiza yake maana mimi naiita miujiza. Sasa hivi ndoa yangu ina miaka sita, tuna nyumba mbili, viwanja vitatu maduka mawili makubwa ambayo tunasimamia wote na vitu vingine vingi. Ingawa majina ni yetu wote lakini hakuna chakwangu hapo.

Mwaka jana mke wangu aliniambia kuwa anataka kuwajengea wazazi wake, nilimuambia poa. Kwetu kuna nyumba kubwa tu ambayo tulijenga na ndugu zangu na nahudumia kama kawaida. Alipoanza kujenga nikaona ndugu zangu kama nyuki, wanavamia na maneno, kunijaza kuwa nimetekwa sijui na maujinga ujinga mengi. Mama naye alianza kumchukia mke wangu mara aniambie kamuongelesha vibaya, mara aniambie hivi mara vile, mara ghafla kabila eti kisa wachaga ataniua sijui nini alikuja hana kitu huku anapendeza.

Baada ya kelele nyingi niliona hii itakuja kuniletea shida. Siku moja nilienda nyumbani, nikaomba kuongea na Mama, alianza kuniambia manano mengi nikamsikiliza sana nikamuambia. “Mama hivi kabla ya kuoa nilikua na nini?” Alinyamaza kisha akaniambia Gari, nikamuuliza na sasa hivi? Akataja vile vichache anavyovijua, nilimtajia na vingine vingi ambavyo havijui akabaki kushangaa. Akaniambia tatizo hushirikishi ndugu zako nikamuambia kwani walishiriki kuzichuma. Nilimuambia;

“Mama nakupenda sana, ila jua kuwa sina akili kama mke wangu nikimuacha yule mwanamke kesho keshokutwa nitakua kama fala flani hivi sina kitu na yule mwanamke hata nikimuacha na laki moja tu mwakani ni milionea. Nauchukuia sana umasikini hivyo kawaambie wanao kuwa wakiendelea kumsumbua mke wangu basi hata kwangu hawatakanyaga. Kujifanya wananiheshimu halafu wanamdharau mke wangu ni unafiki. Mke wangu simuachi, kwao haachi kujenga kama unataka nyumba Mama nilishakujengea hao ndugu watafute vyakwao na wenza wao!”

Mama aliongea sana akilalamika kuwa nimetekwa akili nikamuambia wewe ni Mama yangu hata ukinitukana siwezi kuacha kukuhudumia kwani ni kazi yangu lakini siwezi kumuacha mke wangu, ila waambie wanao kuwa wakimsumbua mke wangu nitasahau kuwa tumezaliwa tumbo moja. Mama aliongea, akaongea lakini niliondoka. Walijua kama natania wakidhani kama nimelishwa limbwata, ile nafika nyumbani mke wangu nakuta hajachangamka, nilimuuliza tatizo ni nini hakuniambia alisema yuko sawa.

Nilihisi kitu nikachukua simu yake, nikaangalia meseji mdogo wangu wakike alikua akimtukana mke wangu kuwa amenilisha limbwata mpaka imefikia hatua namtukana Mama yangu, mara ataondoka tu laana itamshika na mambo kibao. Nilichukua simu ya mke wangu na kumpigia, alipokea hata kabla ya salamu alianza kutukana na vitishi kibao. Nilimuambia kuwa “Inaelekea Mama hakukupa ujumbe wangu vizuri ukauelewa, nilisema atakateendelea kumsumbua mke wangu nitasahau kama ni ndugu yangu, basi wewe nimesahau!”

Nilikata simu na sikumtafuta, ilikua mwaka jana, yeye yuko chuo nilikua namlipia mimi kila kitu nikakata kabisa, nikamuambia sitatoa. Mama akapiga simu akalia lakini nikakataa, mke wangu alinibembeleza sana kumsamehe lakini wapi nilimuambia sitaki. Nilifanya makusudi ili wajue kuwa namaanisha, mwaka huu wote ada aliyelipa ni mke wangu, hawakuniambia lakini najua kwani Mama ndiyo alikua anapiga anamuomba na pia sasa hivi akitaka matumizi anamuomba Mama ili Mama aniombe nimpe.

Najua zinaenda wapi lakini nawacheka tu. Itoe Post yangu kwani mdogo wangu anakusoma sana ajue nimemsamehe ila ajue kuwa mke wangu ni jembe. Ana akili ya Biashara ambayo mimi sina, nina ya darasani tu ila Biashara huyu mwanamke hapana, wakati mimi nikiangalia laki moja naona raundi kadhaa za nyama choma na washikaji , yeye laki moja anaona mtaji wa Biashara. Nimuambie tu mdogo wangu najua bado yeye na Mama wanaamini nimelogwa, hapana ishu sitaki tu umasikini nikimuacha huyu mke wangu anaondoka na mali zake sitaweza kuziendelea na hata nikiwapa nyinyi hamuwezi kuziendeleza!

NB: Kuna wanaume wengi wanafanikiwa kupitia migongo ya wanawake lakini niwachache wanaweza kukubali kama umemkubali huyu basi endelea kufuatilia.
 
Hii tabia ya kucopy na kupaste nyuzi za watu wengine ambazo hata wao sidhani kama ni story zao zimeanza lini humu?kwani ni lazima kila mtu apost au kuna malipo yoyote kwa kupost mimi ndo sijui...pathetic
 
Shikilia hapo hapo, Watu wa bara hili huwa tunapenda Ndugu asifanikiwe, ikitokea unachomoza vikwazo ni vingi.
What a sadist race on earth!
 
Hata kama ya kukopi ila ni nzuri kwa mafundisho. Sasa JF kila mtu ni expert kisa kaisoma. Hii tabia wazungu wangekuwa nayo ya uchoyo ku share sijui hata Shakespeare na Tesla tungewajua..
 
Hahaha hongera boss...Kuna mama mmoja wa kichaga alikuja CapeTown mwaka 2011 wenyeji wake walimkimbia tu alivyoshuka kwenye InterCape(Bus) akitokea Johanesburg,,hakuwapata kwenye simu...Amelala sana nje Salt River..Alikuja kupata kazi kwenye shule ya chekechea kwa mama mmoja wa Kiholanzi kama mpishi..Sasa hivi navyoandika hii post nimemaliza kula Ugali maharage na nyama rost kwenye mgahawa wake.Yani kwa kifupi ni Don yuko vizuri.
 
Mke wangu mimi ni darasa la saba, mimi nimemaliza chuo kikuu ni mhasbu nafanya kazi benki na nina mshahara mkubwa tu. Nilikutana na mke wangu kipindi kaja kuchukua mkopo wa Biashara yake, wakati huo nilikua afisa mikopo. Alinielezea kuhusu Biashara yake, plan zake na namna alivyoanza Biashara nilimuambia ondoka uje kesho. Lakini alipokua anaondoka nilimuita dada mmoja rafiki yangu na kumuambia nitamuoa yule dada, yule ndiyo mke wangu. Hakuamini lakini nilimtongoza nikampata na sasa hivi ni mke wangu.

Ana akili sana huyu mwanamke, kabla ya kumuoa nilikua nisshafanya kazi miaka tisa, nilikua na Gari tena ya mkopo na kiwanja tu. Nilijua sina akili kama yeye hivyo nilimuongezea mtaji kwenye Biashara yake na kumaucha afanye miujiza yake maana mimi naiita miujiza. Sasa hivi ndoa yangu ina miaka sita, tuna nyumba mbili, viwanja vitatu maduka mawili makubwa ambayo tunasimamia wote na vitu vingine vingi. Ingawa majina ni yetu wote lakini hakuna chakwangu hapo.

Mwaka jana mke wangu aliniambia kuwa anataka kuwajengea wazazi wake, nilimuambia poa. Kwetu kuna nyumba kubwa tu ambayo tulijenga na ndugu zangu na nahudumia kama kawaida. Alipoanza kujenga nikaona ndugu zangu kama nyuki, wanavamia na maneno, kunijaza kuwa nimetekwa sijui na maujinga ujinga mengi. Mama naye alianza kumchukia mke wangu mara aniambie kamuongelesha vibaya, mara aniambie hivi mara vile, mara ghafla kabila eti kisa wachaga ataniua sijui nini alikuja hana kitu huku anapendeza.

Baada ya kelele nyingi niliona hii itakuja kuniletea shida. Siku moja nilienda nyumbani, nikaomba kuongea na Mama, alianza kuniambia manano mengi nikamsikiliza sana nikamuambia. “Mama hivi kabla ya kuoa nilikua na nini?” Alinyamaza kisha akaniambia Gari, nikamuuliza na sasa hivi? Akataja vile vichache anavyovijua, nilimtajia na vingine vingi ambavyo havijui akabaki kushangaa. Akaniambia tatizo hushirikishi ndugu zako nikamuambia kwani walishiriki kuzichuma. Nilimuambia;

“Mama nakupenda sana, ila jua kuwa sina akili kama mke wangu nikimuacha yule mwanamke kesho keshokutwa nitakua kama fala flani hivi sina kitu na yule mwanamke hata nikimuacha na laki moja tu mwakani ni milionea. Nauchukuia sana umasikini hivyo kawaambie wanao kuwa wakiendelea kumsumbua mke wangu basi hata kwangu hawatakanyaga. Kujifanya wananiheshimu halafu wanamdharau mke wangu ni unafiki. Mke wangu simuachi, kwao haachi kujenga kama unataka nyumba Mama nilishakujengea hao ndugu watafute vyakwao na wenza wao!”

Mama aliongea sana akilalamika kuwa nimetekwa akili nikamuambia wewe ni Mama yangu hata ukinitukana siwezi kuacha kukuhudumia kwani ni kazi yangu lakini siwezi kumuacha mke wangu, ila waambie wanao kuwa wakimsumbua mke wangu nitasahau kuwa tumezaliwa tumbo moja. Mama aliongea, akaongea lakini niliondoka. Walijua kama natania wakidhani kama nimelishwa limbwata, ile nafika nyumbani mke wangu nakuta hajachangamka, nilimuuliza tatizo ni nini hakuniambia alisema yuko sawa.

Nilihisi kitu nikachukua simu yake, nikaangalia meseji mdogo wangu wakike alikua akimtukana mke wangu kuwa amenilisha limbwata mpaka imefikia hatua namtukana Mama yangu, mara ataondoka tu laana itamshika na mambo kibao. Nilichukua simu ya mke wangu na kumpigia, alipokea hata kabla ya salamu alianza kutukana na vitishi kibao. Nilimuambia kuwa “Inaelekea Mama hakukupa ujumbe wangu vizuri ukauelewa, nilisema atakateendelea kumsumbua mke wangu nitasahau kama ni ndugu yangu, basi wewe nimesahau!”

Nilikata simu na sikumtafuta, ilikua mwaka jana, yeye yuko chuo nilikua namlipia mimi kila kitu nikakata kabisa, nikamuambia sitatoa. Mama akapiga simu akalia lakini nikakataa, mke wangu alinibembeleza sana kumsamehe lakini wapi nilimuambia sitaki. Nilifanya makusudi ili wajue kuwa namaanisha, mwaka huu wote ada aliyelipa ni mke wangu, hawakuniambia lakini najua kwani Mama ndiyo alikua anapiga anamuomba na pia sasa hivi akitaka matumizi anamuomba Mama ili Mama aniombe nimpe.

Najua zinaenda wapi lakini nawacheka tu. Itoe Post yangu kwani mdogo wangu anakusoma sana ajue nimemsamehe ila ajue kuwa mke wangu ni jembe. Ana akili ya Biashara ambayo mimi sina, nina ya darasani tu ila Biashara huyu mwanamke hapana, wakati mimi nikiangalia laki moja naona raundi kadhaa za nyama choma na washikaji , yeye laki moja anaona mtaji wa Biashara. Nimuambie tu mdogo wangu najua bado yeye na Mama wanaamini nimelogwa, hapana ishu sitaki tu umasikini nikimuacha huyu mke wangu anaondoka na mali zake sitaweza kuziendelea na hata nikiwapa nyinyi hamuwezi kuziendeleza!

NB: Kuna wanaume wengi wanafanikiwa kupitia migongo ya wanawake lakini niwachache wanaweza kukubali kama umemkubali huyu basi endelea kufuatilia.
Ni jambo njema kumshukuru mke wako. Ushuhuda wako unatosha ww uwe mfano wa kuigwa kwa baadhi ya Wawume wanao kashifu wake zao hadharani. Nazidi kukuombea kwa wenye moyo kama wa kwako. Kuthamini mchango wa mwenza wako... Tunaoa kwa furaha na mahaba inapotokea tafauti baci tukae kimya na ruzidi kuwasitiri hawa viumbe adimu...
ikitokea story yako ni ya ukweli baci ujue kua mungu ameshakuwekea nuru kwenye mambo yako....
 
Back
Top Bottom