Mke: Wolper niachie mume wangu

Mke: Wolper niachie mume wangu

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Siku chache baada ya kumwanika mchumba' ke , raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambaye tayari amemvisha pete ya uchumba, mambo yamekuwa siyo mambo kwa staa wa filamu za Kibongo , Jacqueline Wolper Massawe kutokana na mke wa jamaa huyo kuibuka na kumtaka amwachie mumewe.

Mkongomani na Wolper .
Chanzo makini kimelieleza Ijumaa Wikienda kwamba , baada ya habari na picha za Wolper na Mkongomani huyo kuripotiwa na gazeti ndugu na hili , mke wa ndoa wa mwanaume huyo alijitokeza na kuvunja ukimya akimtaka mwigizaji huyo aachane na mumewe huyo mara moja kabla hajamchukulia hatua za kisheria kwa sababu ameingilia ndoa yake .

"Unajua baada ya ninyi ( Global ) kuanika picha za Wolper kwenye gazeti na mitandao mbalimbali ya kijamii akivishwa pete ya uchumba na Mkongomani, mke wake ameshindwa kuvumilia hivyo amelazimika kumtumia ujumbe Wolper akimtaka aachane na mume wake kwani kama alikuwa hana taarifa kuanzia leo ( Jumamosi) atambue kwamba huyo mwanaume ni mume halali wa mtu na ana watoto ndani ya ndoa .

"Yaani mke wa Mkongomani amemjia juu Wolper akimtaka amwachie mumewe , ajiweke pembeni mara moja na kama alidanganywa kuwa huyo mwanaume hajaoa , basi atambue kwamba tayari alishafunga naye pingu za maisha , tena kanisani na tayari ana familia ya watoto wawili , haoni sababu ya kumnyamazia maana ameumia sana hivyo anamtahadharisha ili baadaye asije akaanza kulia akisema hajaambiwa ," kilisema chanzo hicho.

MSIKIE WOLPER
Ili kuweka mzani wa habari hiyo , Ijumaa Wikienda lilimtafuta Wolper ili kujua kama ameshayapata malalamiko hayo ambapo alifunguka kuwa , kuna maneno mengi yanazungumzwa juu ya tukio hilo lakini ukweli wa mambo zaidi anaufahamu yeye na mchumba' ke huyo hivyo haoni sababu ya kumwambia kila mtu maana mpaka anafikia uamuzi wa kuvishwa pete tayari walishajadiliana vya kutosha.

"Naweza kusema kwamba ni moja ya historia katika maisha ya mchumba wangu hivyo hata nilipoona hizo picha za mkewe hakuna jambo lililonishtusha kwani tayari alikuwa ameshaniambia juu ya misukosuko aliyoipitia kwenye ndoa yake huko nyuma.

"Hadi anafikia hatua ya kunivisha pete basi watu wanatakiwa kujua tu kwamba kila jambo liko sawa na zaidi wao wanatakiwa kusubiri hadi siku ya ndoa yetu waone kama itafungwa au lah.

"Siku hizi dunia imekuwa kama kijiji hivyo huwezi kuwazuia watu kuongea jambo, mchumba wangu ananijua na mimi ninamjua kwa kina , pamoja na kwamba watu pia wamekuwa wakimletea maneno kuhusu mimi lakini nimemwambia aachane nao kwani hakuna sababu ya kujibizana nao, kwa sababu kila mtu ana uhuru wa kutumia kinywa chake jinsi anavyoweza maana ningekuwa sijui background (maisha ya nyuma ) yake kweli baada ya kuona hizo picha za mkewe na maneno ya watu wanayosema ingeniuma sana.

"Nafikiri watu wanachotakiwa kujua juu yetu ni kwamba Mungu akishapanga jambo kamwe binadamu hawezi kulipangua hata iweje na kwa maana hiyo sasa hata mwanaume akishakupenda ni ngumu kumsikiliza mtu mwingine maana upendo wa mtu ni moyo na nafsi yake mwenyewe ndiyo inayoweza kumuongoza kwa kila hali.

"Watu wameshafanya kila juhudi za kutugombanisha lakini sasa ameshazoea hadi anavichukulia kama burudani tu , hata mimi haya ninayaona kama matangazo ya biashara hivyo hakuna linaloniumiza kichwa ," alisema Wolper.

ETI ANA GUNDU?
Kutokana na kitendo hicho wadau mbalimbali walifika mbali na kudai kwamba mwanadada huyo inawezekana ana gundu kwani ameshakuwa na wanaume tofauti na wengine kumvisha pete ya uchumnba na kutambulishana kwa wazazi lakini ikawa ndivyo sivyo.

"Wolper anatakiwa kujiangalia sana na kumuomba Mungu kwani siyo mara ya kwanza kuwa na wanaume wa watu , kinachowaponza hawa mastaa wetu wana tamaa sana ya fedha ambazo huwasababisha kuwa na mtu kwenye uhusiano bila kumchunguza vizuri, " alisema mdau mmoja mkazi wa Mwenge.

GPL
 
Akili zake mbovu! mwanaume anakuvisha pete bar hakuna wazazi hata hawamjui yeye wala mahariyake
 
Jamani hawa bongo movie hawawezi kua na mwanaume ambae hajawahi kuwa na historia ya ndoa wana drama hawa Kama siyo Serengeti boy basi mume wa mtu
 
Hiyo ndio bongo movie full kuigiza wacha tusubiri part two
 
Mwisho wanakuja sema kiki ya movie.. Mbavu.
 
Akili zake mbovu! mwanaume anakuvisha pete bar hakuna wazazi hata hawamjui yeye wala mahariyake

shoga angu location mbona sio tatizo.........
btw jana ndio alikua anakutana na ndugu wa Cherie wake.
 
Mimi nili shangaa, machozi ya yule pimbi . Kumbe alikua anajutia iba mume wa mtu. Sht..

nifah please..! Majibu yapo clear nw.
 
Last edited by a moderator:
Mwisho wanakuja sema kiki ya movie.. Mbavu.

Hawa akili zao wanazijua wenyewe ni heri uoe barmaid kuliko bongo movie hata ukimkuta.......anabandulia big G atakuambia yuko location.....akili zao wote sawa
 
Kuna wa2 wana kimavi hivi mkongoman gani ambae hana mke kwao wote hawa wakata viuno.....kwao wameoa huku wanakuja saka maisha

Kama ni kinnya basi wolper anacho
anatambulishaga sana insta family,this is my king my commando kipensi bla bla
penzi linaanzia insta na linafia insta
 
Akili zake mbovu! mwanaume anakuvisha pete bar hakuna wazazi hata hawamjui yeye wala mahariyake

Ulitaka wazazi waende kufanyaje?
Mahari ya nini?
Wanaofunga ndoa ni wazazi au Wolper na huyo mwanaume?
Ulitaka wavishane pete wapi?
 
Kama ni kinnya basi wolper anacho
anatambulishaga sana insta family,this is my king my commando kipensi bla bla
penzi linaanzia insta na linafia insta

Shida yao ni maisha y mashindano bongo movie wote wajasiriapapuchi hakuna wife material......na soko lao kwasasa limebuma ndio mana wako kimya
 
Ulitaka wazazi waende kufanyaje?
Mahari ya nini?
Wanaofunga ndoa ni wazazi au Wolper na huyo mwanaume?
Ulitaka wavishane pete wapi?

Ndo taratibu za mira za kiafrika..lazima wazazi wawepo kwenye tukio muhimu kama hilo
 
bongo movie once again. mwenyewe alilia siku hiyo
 
Kama ni kinnya basi wolper anacho
anatambulishaga sana insta family,this is my king my commando kipensi bla bla
penzi linaanzia insta na linafia insta

Sasa mbona anashambuliwa Wolper tu,

Na hiyo midume inayomshambulia mtoto wa mwenzao nao waache ujinga....Mzee Masawe hajasaa mtoto aje kugeuzwa jamfi...kumbafu sao.
 
Back
Top Bottom