Mkeka wa Kimkakati wa Wakuu wa Wilaya washindwa kuzuia shangwe za Mapokezi ya Tundu Lissu

Mkeka wa Kimkakati wa Wakuu wa Wilaya washindwa kuzuia shangwe za Mapokezi ya Tundu Lissu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Taarifa za Kiintelijensia kutoka chanzo cha kuaminika zinadokeza kwamba, kutangazwa leo Ma DC wapya lilikuwa jambo la Kimkakati ili kuwapoteza maboya watanzania na hasa wakazi wa DSM kuhusu Ujio wa Lissu.

Hata hivyo mkakati huo umefeli vibaya sana! Mtoa Taarifa anadai kwamba kufeli kwa njama hiyo ya kizamani kumetokana na timing, kwamba walipaswa kutangaza mkeka huo Usiku wa manane ili watu waamke nao, hata hivyo hakuwa na uhakika iwapo kuwahi kutangaza kama kungesaidia chochote, huku akidai kwamba HAKUNA DC YEYOTE MIONGONI MWA WALIOTEULIWA AU KUACHWA ALIYEFIKIA HATA ROBO YA UMAARUFU WA TUNDU LISSU, amesema kwamba jambo pekee ambalo lingeweza kutikisa ujio wa Lissu ni KUVUNJWA KWA BARAZA LA MAWAZIRI, kitu ambacho hakikufanyika.

Huu ni Ushahidi mwingine wa jinsi ya Utukufu wa Mungu unavyoweza kuzuia nguvu za Shetani.

Natoa wito kwa Wapanga njama hizi za mchongo angalau wawe wanatushirikisha sisi wajuzi wa mambo hayo, vinginevyo wataendelea kuangukia pua.

JamiiForums489093759_384x512.jpg
 
Acha ujinga wewe yaani serikali iogope kuendesha mambo yake kisa Tundu lisu anakuja leo nchini? daah mi mwenyewe huu uzi ndio umenikumbusha kumbe leo ndio anakuja.Hatuna muda huo watu wanaendelea na mishe zao za kutafuta pesa
 
Jiwe alifanya kila namna kuzuia matangazo ya kampeni za Lisu wakati akigombea urais 2020 kwenye redio, TV na mabango lkn alishindwa.

Itakuwa hivi vyeo uchwara vya uDC??

By the way, Nick wa pili mbona haonekani kwenye orodha?
 
Jiwe alifanya kila namna kuzuia matangazo ya kampeni za Lisu wakati akigombea urais 2020 kwenye redio, TV na mabango lkn alishindwa.

Itakuwa hivi vyeo uchwara vya uDC??

By the way, Nick wa pili mbona haonekani kwenye orodha?
hata twitter hatrend anazidiwa na kina dizasta na rapcha nyie mmekalia kuwa na id ishirin ishirin za mchongo
 
Back
Top Bottom