Huyu Dada ametumia barabara tofauti na yule mkenya aliyetembelea rafiki yake Dar. Huyu dada alipofika Arusha, alielekea kulia ili apitie "Central" Tanzania- Babati, Singida, Dodoma, Iringa, Mbeya, hizo ni zaidi ya 1800Km, hajakutana na vumbi wa shimo barabarani.
Yule mkenya mwengine alipitia "Eastern" Tanzania,- Arusha, Moshi, Segera, Chalinze, hadi Dar. Aliporudi alipitia, Bagamoyo, Msata, Segera, Tanga, Horohoro, 1500km bila kugusa vumbi wala shimo lolote.
Kwa ujumla hawa wakenya wawili wametembea jumla ya 2300Km za lami bila kuona shimo hata moja. Hapo ni kama 10% ya barabara za lami Tanzania.