Mkenya apigwa miaka 2800 Kisutu,ni baada ya kuleta ujanja ujanja

Mkenya apigwa miaka 2800 Kisutu,ni baada ya kuleta ujanja ujanja

Mkenya mmoja kwa jina la Murithi amepigwa nyundo (miaka) 2800 baada ya kukutwa na makosa 400 ya utakatishaji wa fedha katika mahakama ya Kisutu.
Nyang'au kama unakuja Bongo kutafuta hela njoo ila uwe unafanya kitu legit maana huku sio sehemu salama kwa mambo yenu ya ajabu ajabu (muulizeni mhindi Sethi),Bongo hatuna tatizo hata kuiweka kaunti moja yote ndani kama mkionekana mnafanya vitu vya ovyo.
Habari zaidi zinafuata wakuu
Tutalipiza kwa kunyonga
 
Askari jela wa Tz walivo vilaza, na zile sare zao za tracksuit. Mohree akikaa ndani zaidi ya miezi kumi atakuwa yeye ndio 'amelalia masikio'. 😀
 
Duh! Bora wange mkata kichwa tu sio kwa adhabu hiyo
 
kila kosa ni miaka mingapi ....je vifungo vinafuatana au vinaambatana???
maswali ya msingi sana!!
 
Aisee hatari sana!!

yule wa juzi kapigwa 81 years makosa 27 kila kosa miaka 3, na nilivyomuona ni kama ana miaka 40+, tuseme 45+81=126 huyo si atakufa maiti yake iendeleze kifungo!!!
 
Kma kila count ni miaka 7 basi atatumikia miaka 7 tu kwa tu sio 2800, kwa mujibu wa sheria zetu za jinai adhabu ya kifungo huenda sambamba
 
Hiyo ni 7 saba, wakati mwingine sheria ni kama mnataniana tu, amefungwa miaka 2800 kwa makosa 400, kwahiyo chukua 2800÷400, kila kosa ni miaka 7,
Kwahiyo kama atatumikia makosa yote kwa pamoja, maana yake kila mwaka anatumikia makosa yote 400, kwahiyo ndani ya miaka saba atakuwa amelamba kifungo cha miaka 2800,
So funny!!
 
Si bora wangemfunga maisha tu, maana hiyo miaka hawezi maliza, labda apate msamaha
 
Hiyo ni 7 saba, wakati mwingine sheria ni kama mnataniana tu, amefungwa miaka 2800 kwa makosa 400, kwahiyo chukua 2800÷400, kila kosa ni miaka 7,
Kwahiyo kama atatumikia makosa yote kwa pamoja, maana yake kila mwaka anatumikia makosa yote 400, kwahiyo ndani ya miaka saba atakuwa amelamba kifungo cha miaka 2800,
So funny!!
Na kama siyo flat basi kosa lenye kifungo kirefu zaidi ndiyo hutumikiwa.
 
Kaburi lake litafungwa pingu hata akifa...!
 
Yaani hiyo miaka 2800
Akifa yeye atakuja mwanaye atafungwa atakuja mjukuu atafungwa na kitukuu atafungwa kilembwe atafungwa mpaka 2800 miaka itimie.

Chezea wabongo wewe, siyo watu kabisa.

[emoji4]

Akifa kaburi lake litawekwa pingu za zege na miguu inafungwa kwa pingu imara![emoji1]
 
Back
Top Bottom