joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Tukiweka ushabiki kando wa Kenya na Tanzania, ni wazi kwamba wakenya wengi wanaikubali sana Tanzania, hii inathibitishwa na jinsi wakenya wengi hasa wale wasomi wanavyoizungumza Tanzania katika mijadala mbalimbali huko kwao.
Katika mijadala mbalimbali katika TV, Redio au mijadala ya wazi, huwa wanaitumia Tanzania kama mfano mzuri wa kuigwa na Kenya katika utendaji wa Kazi.
Ninadhani hili ni jambo zuri, nikimaanisha kuiga mambo mazuri kwa jirani yako. Hongereni sana kwa wale wenye wivu wa maendeleo.