Mkenya Joy afariki Saudi Arabia baada ya kuanguka akiwa anacheza na Mtoto wa Mwajiri wake

Mkenya Joy afariki Saudi Arabia baada ya kuanguka akiwa anacheza na Mtoto wa Mwajiri wake

OwadeKuya

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
535
Reaction score
312

​
Mwanamke Mkenya anayetambulishwa kwa jina la Joy ameripotiwa kufariki nchini Saudi Arabia baada ya kuanguka ghafla alipokuwa akicheza na mtoto wa mwajiri wake.

Video inayosambaa mitandaoni inaonyesha Joy akicheza kwa furaha na mtoto huyo ndani ya nyumba ya mwajiri wake kabla ya ghafla kuanguka chini na kupoteza fahamu.

Muda mfupi baadaye, mtu mwingine anaonekana akiingia katika chumba hicho baada ya tukio hilo.
Kwa mujibu wa maelezo yanayoambatana na video hiyo, Joy alifariki kufuatia tukio hilo, ingawa mazingira kamili ya kifo chake na chanzo cha kuanguka kwake bado hayajathibitishwa.

Tukio hilo limeibua huzuni na maswali kuhusu usalama na ustawi wa Wakenya wanaofanya kazi za nyumbani katika mataifa ya Ghuba.
 
Kasongo anasemaje kuhusu hili tukio?
 
Kupima afya mara kwa mara ni muhimu sana , vifo vya hivyo kwa miaka ya karibuni vimekua vingi sana
 
Back
Top Bottom