Nimekuwa observer kwa hii thread, hakika nimeona michango yenu yenye haja. Lakini swali langu kwa hawa wanaodai facebook kuwa chanzo cha ndoa nyingi kuvunjika, kwanza je takwimu hizo zipo?.....tupeni, pili facebook yenyewe kama social networking, ina specialty ipi, kuliko zingine mambazo zilikuwepo na watu walifanya social networking kwa muda mrefu tu, mbona hayo hatukuyasikia. Bado sielewi vizuri hapa. Kuwepo kwa facebook, au kutokuwepo bado watu wameweza kuwasiliana tu, na kama nia ipo ya kumpata ex, hata kama angekuwa wapi still ungeweza kumpata. Na je, kwa mtazamo huo, ina maana wale exes ambao hawana hata account ya hiyo facebook, hawawezi kupata, au kuwasiliana. Naomba mnijuze waungwana.