Mkeo ni wa kundi gani kati ya haya?

Mkuu siwezi uza ramani ya vita kwa adui. Subiri tu kugawiwa kadi ya harusi, uje uhudhurie sherehe. Tena sitachangisha mtu mchango wa harusi...
Hahahahahaha hapo kweli utakuwa umeoa
 
Huyo mkeo anafaa sana kuanzisha nae TV Series. Bora umemjulia aisee! Maana ukishindana nae unakula K.O mapema sana.
 
Sijui why huwa hawakubali makosaa yani Never ever...!!
 
.....................Sikuwahi kuchunguza sana kuhusu mabadiliko niliyokuja kuyaona miaka michache baada ya ndoa but nachokumbuka mwanzo ama akini-ectia ama ni mabadiliko tu yalitokea ila alikuwa smart sana kwenye maamuzi na uelewa (sisemi kwamba sasa hivi hayupo smart) ila amenifanya nizidi kuishi nae kwa akili sana.

Nachoweza kusema na kwa experience yangu ndani ya ndoa miaka 8 sasa ni kwamba kadiri mnavyoongeza familia ndivyo na tabia za mkeo zinavyoanza kubadilika,(haijalishi ni understanding au non-understanding)hakuna siku atakutukana ila baadhi ya huduma ulizokuwa ukipewa zamani bila kuuliza itakubidi wewe mwenyewe uanze kujifanyia na wala usithubutu kuuliza omba uwe na hekima ya kujua mapema maana ya mabadiliko hayo lah hukujua utaitumbukiza ndoa kwenye vurugu,personally miaka ya mwanzo akinitengea maji ya kuoga,kuninyooshea nguo,kunipakulia chakula nikirudi home anapokea kama mkononi nina kimfuko au bag atakuja kupokea ila baada ya kupata mtoto wa kwanza hiyo ya kuwekewa maji ya kuoga na kuandaliwa nguo zilikufa nikabaki na favor mbili,kupokewa mzigo mwenyewe nilikataa nikaona kama utumwa sasa tuna watoto wawili hii ya kupakuliwa chakula muda wowote naona itakufa.

Obviously malalamiko mengi ya wanaume kwenye ndoa hutokana na huduma fulani kukatwa ghafla na majibu yasiyotegemewa kutoka kwa wake zao pale wanapouliza sababu,nilichogundua;anakuwa busy zaidi na watoto so hawezi kuacha kumlisha mtoto akakuandalie wewe maji ya kuoga,hawezi kuacha kumnyonyesha mtoto au kumuandaa mtoto awahi school bus akakunyooshee nguo also hawezi kuacha kumuogesha mtoto akakupakulie chakula mezani sasa ukiwa macho juu juu utataka kuhoji “inakuwaje zamani ukifanya hiki na hiki mbona sasa hivi hunifanyii” jibu utakalopewa hapo ndo litakaloamua hatma ya ndoa yenu,binafsi nachoshukuru niliweza ku-match na mabadiliko haya mapema na nachowashauri mnaotaka kuingia kwenye ndoa jueni mke siyo kwa ajili ya kukuhudumia wewe kwa kila kitu wanaopaswa kuhudumiwa kwa kila kitu na yeye wewe pia ukishiriki ni watoto wenu mtakaowazaa.

Well.....vurugu zipo na ieleweke tukubali au tukatae wanawake % kubwa wanafanana akili awe amesoma au hakusoma hakuna mwanamke anayekataa au anayekubali kosa kizembe,ni “kuishi nao kwa akili tu” ukiijua sentence hii na ukakubali ikuongoze kwenye arguments na mkeo ndoa utaiona tamu tofauti na hapo ni pigo.
 
Kuna uwezekano wa kuwa namba moja ili nikuoe? [emoji12][emoji12][emoji12]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] kuna mtu alikuwa hana mume, basi akawa anasema nikipata mume mimi...nitampetipeti, nitamnyenyekea, sitowahi 'kumuintarapti' akiongea, sitowahi kumnyima. Alipoolewa sasa utadhani ni mwingine....nilichojifunza mtu ukiwa single kwa vyovyote utajiweka namba moja, ingia ndoani sasa.
Kwa hiyo BAK mimi nipo namba moja. Leta tu mahari hiyo
 
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122] well said
 
Hahahahaha umeswitch back to number one so fast without even asking any questions 😂😂😂😂😂 ila kwenye ndoa mitafaruku haikosi ila kikubwa ni namna ya kukaa chini na kuimaliza mitafaruku husika. Wengi hili linawashinda na ndiyo sababu siku hizi ukilinganisha na ndoa za Baba zetu ni miaka miwili/mitatu ndoa imeshajifia.

 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] kiukweli sidhani kuna mtu anayependa kuwa namba mbili, inatokea tu
 
Mke wangu yuko kundi la kwanza ila ana mambo flan flan ambayo nnajitahd kuyapuuza sababu siku nikiyafuatilia kiundani nadhani itatakiwa niwe nishapata mbadala wake.
 
Umeongea vizuri,kiume kabisa Kuna mtu I wish asome ,Mana anajuaga mke Ni msukule
Yani mwanaume ukiwa na hizi akili za huyu Kaka utaishi miaka mingi anaona changes kwa mkewe Ila anajuwa fika lazima iwe hivyo sababu ya majukumu na watoto kuongezeka .
Kunywa soda kwa mangi
 
You are a true definition of a husband
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…