Mkesha wa Vuka Kabla ya Kuvuka

Mkesha wa Vuka Kabla ya Kuvuka

Dadakidoti

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2024
Posts
399
Reaction score
1,409
SALAAM

Mada yahusika hapo juu.
Jana kulikuwepo mkesha ulioandaliwa na huduma ya Arise and Shine chini ya Mtumishi Mwamposa.

Nilikuwa nikufuatilia matukio nikiwa nyumbani kupitia TV. Kilichonichosha na kunitoa kwenye reli kabisa ni pale mkuu wa mkoa alipopewa nafasi ya kusalimia waaumini.

Alinichosha zaidi aliposema kuwa huwa anamkumbuka dada wa Bukoba akimaanisha Saida Karoli aliposema anapenda wimbo wake wa mwenye wivu ajinyonge. na kuanza kuimba wimbo huo.

Nimejiuliza maswali mengine:

1. Kwanini mtu Mkubwa na cheo chake aongee vitu kama hivyo?

2. Je, madhabahuni si mahali pa watu kuponya nafsi zao? inakuwaje unaongea vitu kama vya kupiga majungu?

3. Aliwaza watu watalipokeaje?

4. Hakuwa na kitu cha kuongea si angekaa kimya?

Muwe na siku njema niliyemkosea anisamehe.
 
Tumwambie apige maombi timu zote za Tanzania (Yanga na Simba) ziende robo fainali
 
Ukiamini ama kuaminishwa kwamba watawala wa nchi hii wako serious na wanachokifanya basi utapata tabu asana..harakati zao zote wewe chukulia kama drama tu, utaiponya afya yako ya akili.
 
SALAAM

Mada yahusika hapo juu.
Jana kulikuwepo mkesha ulioandaliwa na huduma ya Arise and Shine chini ya Mtumishi Mwamposa.

Nilikuwa nikufuatilia matukio nikiwa nyumbani kupitia TV. Kilichonichosha na kunitoa kwenye reli kabisa ni pale mkuu wa mkoa alipopewa nafasi ya kusalimia waaumini.

Alinichosha zaidi aliposema kuwa huwa anamkumbuka dada wa Bukoba akimaanisha Saida Karoli aliposema anapenda wimbo wake wa mwenye wivu ajinyonge. na kuanza kuimba wimbo huo.

Nimejiuliza maswali mengine:

1. Kwanini mtu Mkubwa na cheo chake aongee vitu kama hivyo?

2. Je, madhabahuni si mahali pa watu kuponya nafsi zao? inakuwaje unaongea vitu kama vya kupiga majungu?

3. Aliwaza watu watalipokeaje?

4. Hakuwa na kitu cha kuongea si angekaa kimya?

Muwe na siku njema niliyemkosea anisamehe.
Kama uliweza kufuatilia kwenye TV una tofauti gani na hiyo misukule ya Mwamposa?
 
Ndiyo shida ya viongozi wa
kuteuliwa hiyo mkuu, Imagine kungekuwa na utaratibu wa mkuu wa mkoa kuchaguliwa na wananchi pumba zingekuwa chache!
 
Huyo kipara komwe sio mzima kichwani, asamehewe tyuuh.
Na anavopiga ulabu, ndo anazidi kuzimisha fusse za oblangata yake.
 
Back
Top Bottom