Kule kwenu musoma mafuriko balaa, watu hawana pa kwenda wanang'ang'ana na nyumba zao huku zimezingirwa na maji ndani na nje. Cha ajabu watu wanalala huku maji yako chini ya kitanda, ikiongezeka mvua hivyo vitanda vitafunikwa na maji. Sisi kwetu huku mafuriko tunayasikia na kuyaona kwa wengine hatuna mvua za kutujazia maji mitaani yanaishia maboni na kutafuta njia za kwenda maziwani na mabwawani. Tumuembe Mungu atupe mvua za kutosheleza mahitaji yetu zisizidi kiwango cha juu nyumba zetu za tope zitadondoka