Mkimbizi aliyejengewa sanamu

Mkimbizi aliyejengewa sanamu

SportSpapeR

Member
Joined
Sep 20, 2015
Posts
7
Reaction score
4
KIJIWE CHETU

MKIMBIZI ALIYEGEUKA MFALME BARCA

Huwa nina Kamsemo Kangu nasemaga ivi, "you can Find a Peace anywhere, but you can't find a love Everywhere" unaweza kukuta amani Popote Pale lakini huwezi kupata upendo kila mahali....
**********************

Wakati fulani wakimbizi hukimbia ili kutafuta amani na sio upendo, ila aman yao inakuwa ya kudumu hasa pale wanapopata pendo. Kama Kubala asingepata Upendo Pale Barca huenda asingekuwa shujaa wao. Kubala hakuwa Mhispania alikuwa mtu kutoka Hungary lakin alikimbilia Italy mwaka 1948 kutafuta amani.
****************************************

Maisha ya Mchezaji huwa yanahitaji amani, lakini kama atakosa Upendo basi sahau kuhusu Mafanikio yako! Mfano Tu Arjen Roben alikosa upendo Madrid lakin aman alikuwa nayo ila akaona anahitaji Upendo. Jose Mourinho kwa sasa yupo kwenye kilio, hana Aman, lakin bado anapendwa na Mashabiki wake, wakati anatoka Madrid alisema naenda mahala ambako napendwa bila kujali kama atapata aman au la!
*************************************

Mnamo Mwaka 1927 tarehe 10 julai alizaliwa mchezaji bora kabisa wa Muda wote kule Hungary maeneo ya Budapest Ajulikanae kama Laszlo Kubala. Miaka 21 baadae huyu jamaa alikimbilia Roma Italia. Klabu ya Pro Patria iliona imchukue mwaka 1949, ingawa alicheza mechi za kirafiki tu maana FIFA ilimfungia kucheza mechi za ushindan baada ya Hungary kulalamika kuwa hakuwa na kibali maalum kufanya kazi Italia.
**************************************

Joseph Samiter aliyekuwa katibu wa Barcelona wakati ule alimchukua kinda huyo tarehe 15 june 1950. Mechi yake ya kwanza dhidi ya Ossasuna alitupia Goli moja kwenye ushindi wa 4-0, huyu jamaa alijunga na wakali kama Basora, Cesar, Moreno na Manchon na klabu ilitwaa makombe matano ndani ya mwaka mmoja na nusu kuanzia 1951-53. Na hii ilitajwa kuwa moja ya safu za ushambuliaji hatari zaidi Duniani kwa wakati ule.
*******************************

Alicheza michezo 345 na alifunga magoli 271 bonge moja la Rekodi na alishinda tuzo tano za silva, makombe manne ya ligi, kombe la latini, fairs cup, makombe matano ya spanish cup, makombe mawili ya Eva Duarte. Baadae alikuwa kocha klabuni hapo mwaka 1961 mara baada tu ya kustaafu na pia aliondoka mwaka 1963 na mwaka 1980 alirudi ila hakupata mafanikio yoyote makubwa! Kubala alifariki mwaka 2002 hapo hapo Barcelona na amejengewa sanamu hao Nou Camp mwaka 2009. Hapa ndipo nasema wakati anatafuta aman alikutana na Upendo Wa Ajabu, huenda alikosa upendo nyumban kwake lakin amepata aman ya kudumu maishan mwake
 
Back
Top Bottom