Mkioa/Kuolewa mtulie kwenye ndoa

Mkioa/Kuolewa mtulie kwenye ndoa

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
1,842
Reaction score
6,087
Copy and paste kutoka kwenye page ya HIV living postive instagram.

"Naitwa XXX naishi iringa naomba msaada napitia kipindi kigumu sana sijui nianzie wapi nina stress nyingi sana nimeolewa na nimeishi na mtu wangu kwa miaka miwili sasa, tulipima pamoja na tulikua negative 2022, Mwaka jana nilibahatika kushika mimba na niliudhuria clinic zoote nikawa napima na nikawa na hali nzuri tu.

Mwezi wa nne mwanangu alianza kupata vipele vipele mara kwa mara kila tukienda hospital wanakosa kujua chanzo, mpaka baadae doctor akanambia tupime ukimwi, kweli doctor tulipima na mimi nikakutwa na UKIMWI.

Naogopa kumwambia mwenza wangu kuhusu hali hii, maana yeye kazini kwake huwa wanapimwa mara kwa mara, na hata juzi tumepimwa yuko salama, najaribu kuwaza UKIMWI nilipatia wapi?.

Naomba niwe mkweli doctor kuna kipindi nilisafiri kwenda njombe, nikakutana na boy friend wangu wa zamani, ikatokea tu tukakaa naye siku 5, japo yeye anasema yupo salama, nilimuuliza kama yeye anajua hali yake akasema kapima na yuko salama.

Pia nilikua na mbaba Mwingine yupo Iringa tulitumia kinga bao la kwanza, lakini la 2 na 3 nahisi alivua condom sasa niko njia panda ni nani alienipa huu ugonjwa, naogopa kumwambia mme wangu.

MY TAKE.
Ni vyema wakuu mtu ukishaoa/kuolewa utulie na mtu wako majuto ni makubwa mno, pia mambo kama hayo ndio yanasababisha vijana wasifikiri kuoa kabisa, hakuna kitu kinawapa mawazo wanaume kama kufuga malaya na kuweka ndani.

Credit: Doctor lawi instagram, HIV LIVING POSTIVE.
 

Attachments

  • Screenshot_20240529-091926.png
    Screenshot_20240529-091926.png
    932.1 KB · Views: 26
  • Screenshot_20240529-092017.png
    Screenshot_20240529-092017.png
    1 MB · Views: 26
Unapata wapi nguvu ya kukutana kimwili na ex wako?
Aisee mimi tukiachana ndio moja kwa moja, sitaki kuwa mtumwa wa ngono kijinga hivyo.

Mpaka tunaachana ni dhahiri hatukupangikiwa kuwa pamoja! Kuendekeza upuuzi tu.
Halafu tukisema humu mwanamke wa kuoa ni bikra pekee tu na maana hana huu upuuzi wa maex... wanawake mnang'aka
 
Back
Top Bottom