Mkiristo anayedai kumpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wake bila kutahiriwa nyama ya govi lake huyo ni mpagani na kafiri

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Moderator naomba Uzi huu uache ujitegemee tafadhali

Wadau hamjamboni nyote?

Ni vema tuelezane ukweli kuwa huwezi kuwa Mkiristo wa kweli uliyempokea Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wako bila kutahiriwa

Makasisi, wachungaji na maaskofu tuwahimize waamini watahiriwe nyama za magovi Yao kabla ya kubatizwa au kupokea ekaristi takatifu

Ni wapagani na makafiri pekee ndiyo wasiofanyiwa tohara

Tafakuri ya kina kwa wenye hekima

Mwanzo 17:12 2 Mtoto wa siku nane atatahiriwa kwenu, kila mwanamume katika vizazi vyenu, mzaliwa nyumbani, na mnunuliwa kwa fedha, kila mgeni asiyekuwa wa uzao wako.

Mwanzo 17:13 3 Mzaliwa nyumbani mwako, na mnunuliwa kwa fedha yako, lazima atahiriwe; na agano langu litakuwa katika mwili wenu, kuwa agano la milele.
 
Acha ujinga! Kutahiriwa kimwili ni jambo la kijamii. Ukristo ni kutahiriwa moyo.
 
Katika Agano Jipya, suala la kutahiriwa linazungumziwa kwa mtazamo mpya, tofauti na jinsi lilivyoelekezwa katika Agano la Kale. Kutahiriwa kulikuwa ishara ya agano kati ya Mungu na Abrahamu (Mwanzo 17:9-14), lakini katika Agano Jipya, mafundisho yanahama kutoka kwa tohara ya kimwili kwenda kwa tohara ya kiroho.

Mambo Makuu Kuhusu Kutahiriwa Katika Agano Jipya

1. Tohara si sharti la wokovu
Mtume Paulo alifundisha wazi kwamba wokovu haupatikani kwa matendo ya sheria, ikiwa ni pamoja na tohara, bali kwa neema kwa njia ya imani katika Kristo Yesu:

"Kwa maana kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa si kitu, bali kushika amri za Mungu." (1 Wakorintho 7:19)

"Kwa maana katika Kristo Yesu, kutahiriwa hakufai kitu, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo." (Wagalatia 5:6)



2. Tohara ya kweli ni ya moyo, si ya mwili
Paulo anafundisha kuwa tohara halisi ni ile ya moyo, inayoletwa na Roho Mtakatifu, si tohara ya kimwili inayofanyika kwa mikono ya wanadamu:

"Kwa maana yeye si Myahudi aliye wa nje tu, wala tohara si ile ionekanayo katika mwili tu. Bali yeye ni Myahudi aliye wa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu." (Warumi 2:28-29)



3. Mkazo ni juu ya tohara ya kiroho kupitia Kristo

"Katika yeye mlitahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mikono, kwa kuuvua mwili wa dhambi ya mwili, kwa tohara ya Kristo." (Wakolosai 2:11)
Hii inamaanisha kwamba waamini wanapaswa kumwelekea Kristo, ambaye huondoa dhambi zao, badala ya kutegemea desturi ya kimwili ya tohara.



4. Mkristo hana ulazima wa kutahiriwa
Katika kitabu cha Matendo ya Mitume 15, swali la tohara lilijadiliwa na mitume katika Baraza la Yerusalemu. Uamuzi wao ulikuwa kwamba watu wa Mataifa wasilazimishwe kutahiriwa ili kuwa Wakristo:

"Basi sasa, mbona mnamjaribu Mungu kwa kuiweka nira juu ya shingo za wanafunzi, ambayo wala baba zetu wala sisi hatukuweza kuichukua? Lakini twaamini kwamba tumeokoka kwa neema ya Bwana Yesu vile vile kama wao." (Matendo 15:10-11)




Hitimisho

Katika Agano Jipya, tohara ya mwili si sharti la wokovu. Mkazo umewekwa juu ya tohara ya moyo—kubadilishwa kwa ndani na Roho Mtakatifu kupitia imani katika Kristo. Badala ya kushikilia desturi za Sheria ya Musa, waamini wanahimizwa kuishi kwa imani katika Kristo
na kushika amri za Mungu kwa upendo.
 
Kichwa kimekuumuka kikiwaza Govi la dushe😂
 
1 KOR. :7:19
Kutahiriwa si kitu, na kutokutahiriwa si kitu bali kuzihifadhi amri za Mungu

GAL. :5:6
Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo

KOL. :3:11
Hapo hapana Myunani wala Myahudi, kutahiriwa wala kutokutahiriwa, mgeni wala mshenzi, mtumwa wala mwungwana, bali Kristo ni yote, na katika yote.
 
Kupata vichekesho kama hivi andika

UPUUZI KWENDA no 15777
 
Hao walioleta dini africa wengi ni magovinda
 
Wewe ndiyo Yesu hadi upangie watu kiasi hiki? Mungu ni mjinga hadi awake hilo govi?
 
Paulo alitahiriwa?
 
Umekunywa BUTUA WEWE
Philippians 3:5
[5]Circumcised the eighth day, of the stock of Israel, of the tribe of Benjamin, an Hebrew of the Hebrews; as touching the law, a Pharisee;
Nalitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benyamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo,
 
Kwa fundisho la Paulo kuwa wokuvu haupatikani kwa matendo ya Sheria. Nadhani linaruhusu Kila aina bata, uchafu na uovu!

Ni fundisho ambalao halikueleweka na walengwa. Paulo hakutaka watu wapuuze Sheria, Bali waende mbele zaidi. Sheria ndiyo, ila na usafi wa moyo!

Kwa Waislamu Wana categories hizi..
1. Dini
2. Imani
3. Ihsani.

Paulo alikuwa anafundisha ihsani, usafi wa roho bila kupuuza Sheria!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…