Mkishindwa kushindana, muungane

karv

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2019
Posts
1,802
Reaction score
3,253
Katika siku ambayo Dauda ameongea maneno ya hekima na busara basi ni jana YANGA kuna haja kubwa ya kujifunga kutoka kwa watani zenu

"Kuna wakati wengine wakae na Viongozi wa Simba mnajadiliana tu kuwa imewezekana vipi kuwa na mwendelezo kwa misimu mitano, ipi siri! Nanyi mnajifunza

Real Madrid na Barcelona wamesaini mkataba wao wa kutoingiliana sehemu baadhi za usajili

Mkishindwa kushindana, MUUNGANE

[emoji1488] Shaffih Dauda [emoji1488]
 
Shafii atumikie adhabu ya kusambaza habari za uongo ache janja janja.
 
Mmepigwa gape la point 8 kwenye ligi, mmezidiwa kila angel ya ubora kitakwimu bado mnabweka kama mbwa aliyekoswa kugongwa na gari barabarani, mmeshinda ushindi wa Rose muhando dhidi ya berkane mnajiona mmemaliza kila kitu duniani maneno meeengi utadhani mmechukua kombe ni ayawani pekee ambae anaweza kufungua mdomo na kuifananisha yanga ya msimu huu na simba kiubora, ukibisha tuletee takwimu ndo zitazungumza nani ni bora zaidi ya mwenzake ayo mengine ni maneno ya wakosaji wasiojielewa
 
Yanga ni kama chizi aliyebakia uchi kwenye soko la kijiji saa sita mchana.Watu wanamuangalia alivyobaki na shanga kiunoni.
 
Yanga kwa sasa anaongoza ligi ya Tz kwa tofauti ya point nane, na kuna dalili ya kuweza kuchukua ubingwa,hayo nayo ni mafanikio, wana haki ya kujivunia.

Simba kwa sasa anaongoza kundi kwenye mashindano ya shirikisho la Afrika, na huenda akavuka kuingia hatua ya robo fainali, nusu fainali, fainali na hata kuchukua ubingwa, hayo pia ni mafanikio, wana haki ya kujivunia.

Sina tatizo na Yanga au Simba kujivunia kile walichofanikiwa mpaka sasa, huwa napata tatizo kwa wote hao kubeza, kukejeli au kushindwa kuona mafanikio ya mwenzake.

Tubadilike sasa.
 
ona hii kisinda inavyopovuka

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…