Mkitaka uraia pacha basi rahisisheni taratibu za watu kupata passport na kutoka nje ya nchi

Mkitaka uraia pacha basi rahisisheni taratibu za watu kupata passport na kutoka nje ya nchi

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Matajiri na wanasiasa wanataka uraia pacha utakao wafaidisha wao na watoto wao tu. Toka uhuru, wao ndiyo wenye uwezo wa kupata passport na kwenda nje kwa urahisi. Watoto wa masikini wamejazwa vikwazo kibao juu ya kutoka nje ya nchi. Yaani vikwazo vilivyopo ni ngumu watoto wa kimasikini kuvishinda.

Kama mnataka urai pacha, na mnasema utatufaidisha wote, basi vikwazo kwenye kutoka nje ya nchi na kupata passport viondolewe. Mtu akija na namba yake ya NIDA na kama 30k apewe passport yake.

Zaidi ya hapo huu uraia pacha utakuwa kwaajili ya wanasiasa, matajiri na uzao wao.
 
Rais atoe tangazo tu MAMBO YA NDANI WAHAKIKISHE KILA MTANZANIA ANA PASSPORT YA KUSAFIRIA...awape mwaka mmoja..

Huko USA amuombe BIDEN wabongo wawe na Free viza, aende EU pia afanye hivyohivyo, aende Canada afanye hivyo, aende Japan na Korea kusini afanye hivyo hivyo pia
 
Huyu huyu au mwingine?

Hivi najiulizaga ila sipati jibu, hivi akisema nimeshindwa anahisi ataoneka mjinga au
 
Kwa kweli mimi Dunia huwa naiona kama moja tu hakuna cha nchi wala nini
Woga ndio unawafanya mhangaike
Nimesafiri nje miaka zaidi ya 40 na nimetumia passports aina tofauti

Najua kwa wabongo ni ngumu kufikia maamuzi hata kuhama mkoa mpaka mkoa labda ahamishwe kikazi ila bila hivyo anaweza kukaa sehemu moja mpaka anakufa

Dunia hii hii unayoweza kupata hata passport ya Bangladesh na ukasafiri nayo [emoji1] [emoji1787]

Diaspora mtawachukia bure hawana shobo wala
Kwanza hao mnaowasema ni matajiri na wanasiasa wengi wana passports za nje na ndani na ni wachache sana hawajai hata kiganja

Ila sisi wabeba box ndio tupo wengi na laiti mgejua tuna uwezo gani wa kuunyanyua uchumi msingekuwa mnabeza

Imagine nilituma tractors 6 na kuziuza sasa kama ningekuwa na uraia pacha hapo ningelima mashamba ekari ngapi?

Na je huyo ambae kwao kuna milima ya Mawe na kina mama wanavunja kwa nyundo kila siku mpaka wanaumia
Unafikiri huyo Diaspora hana uwezo wa kununua machine kubwa ya kuvunja mawe?

Najua wengi watabeza ila ukweli ni kwamba nchi ambazo wamekubali dual citizenship wanafaidi sana na watu wao waliopo nje maana wamewekeza kama wazawa na sio foreigners kama mnavyotuita
 
Rais atoe tangazo tu MAMBO YA NDANI WAHAKIKISHE KILA MTANZANIA ANA PASSPORT YA KUSAFIRIA...awape mwaka mmoja..

Huko USA amuombe BIDEN wabongo wawe na Free viza, aende EU pia afanye hivyohivyo, aende Canada afanye hivyo, aende Japan na Korea kusini afanye hivyo hivyo pia
Duuh, free entry, free visa for eveeerry body..?
 
Ukiwa na documents zote muhimu zinazohitajika wakati wa kuomba PASSPORT, utaipata bila tabu yyte.
Na sasa hivi utapata withini 2 weeks !

Lakinibpia kuna documents nyingine ,naoana hazina msingi sana zinwakwamisha baadhi ya watu.
 
Back
Top Bottom