Mkiwa mmekaa zenu Maskani halafu Mama akampa Mtoto Hela akanunue Kitu Dukani kisha akiwaona anampa Maelekezo haya Mtoto huwa anamaanisha nini?

Mkiwa mmekaa zenu Maskani halafu Mama akampa Mtoto Hela akanunue Kitu Dukani kisha akiwaona anampa Maelekezo haya Mtoto huwa anamaanisha nini?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Unakuta mmekaa zenu Maskani ( Kijiweni ) tena hasa Kipindi hiki Joto lililopo Jiji na Kune Boy ( Dar es Salaam ) ili mlipunguze Mwilini mwenu unakuta Mama anamtuma Mtoto wake Dukani kununua Kitu lakini akiwaoneni tu nyie mmekaa anaongea kwa Msisitizo na Sauti ya juu kabisa huku akiyasema haya maneno nayanukuu hapa...." Mwanangu shika vizuri hiyo Shilingi Elfu Kumi nenda pale kwa Mangi mwambie akupe Unga na Mafuta ya Taa. Kuwa Mwangalifu huko njiani Hela isije ikapotea kwani sasa Maisha ni magumu na ufanye upesi urudi kwani kuna wengine wakiingalia tu hiyo Hela inawafuata Mifukoni mwao moja kwa moja"......mwisho wa Kunukuu / Kumnukuu huyu Mama.

Na huyu Mama akiwa anayaongea haya maneno yake halafu Macho yake yote Makubwa kama Kende za Fisi yakiwa yanatizama Kwenu humaniisha nini?

1. Je, anamtahadharisha kuwa Sisi wa Vijiweni ni Vibaka?
2. Je, anatuomba na Ulinzi kwa Mwanae anapokuja Dukani?
3. Je, anatutafutia tu sababu ili tukasirike na tumjibu vibaya?
4. Je, anataka kutuonyesha kuwa Yeye Maisha yake ni mazuri?
5. Je, anataka kutufanya Sisi ni Washukiwa wake wa Kwanza kama Mwanae akiipoteza Hela aliyompa?
6. Je, labda kuna Mtu Mmoja kati yetu ana rekodi nae ya Uwizi hivyo anatuma Salamu ( Ujumbe ) Kwake kinamna namna?
7. Je, pengine kati yetu tuliokaa Kijiweni ( Maskani ) labda kuna Mpenzi wake hivyo anataka amuongezee Mwanae Pesa?
 
Maswali yote ni majibu
 
Maana yake nyie ni vibaka mkuu. Anawaona kwamba hamna mbele Wala nyuma ndiyo maana.

Pia mwanaume unaendaje kukaa kijiweni aisee? Kwani hauna hata mradi wa kwenda kusimamia mkuu?

Kadhalika, mtoto wa kiume unalalamika joto? Hahahah
 
Huyo mpuuzi hana kazi ya kufanya
 
Back
Top Bottom