Mko wangapi kwenu mnaotumia mitandao ya kijamii?

Mko wangapi kwenu mnaotumia mitandao ya kijamii?

LA7

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
655
Reaction score
2,369
Sio kwamba najisifia la! hasha! Kuna wakati huwa natamani hata kaka yangu au dada yangu au ndugu wengine wa karibu waone au wasome nilichokiweka mtandaoni lakini inakuwa ngumu.

Katika familia yangu baba ana wanawake wa nne hivo watoto jumla tulio hai tupo 27, mimi ni wa 5 upande wa mama yangu katika watoto 8 na ndo mimi pekee yangu kwa familia yetu ninaye jua hata kutumia JF.

Lakini sababu inayochangia hawa ndugu wengine kuwa hivyo labda pia maisha ya kijijini kwa saana, ukiangalia pia mambo ya internet vijijini ni taabu japo si mimi pekee niliyetembea mjini.
 
Nunua smart phone 27 harafu pita kwa kila mmoja mwachie moja nawe utakua nao pamoja uko social network l.

Amani iwe nawe
 
Sometimes natamani kujua watu wenye familia kubwa mnaishije maana hizi ndogo ndogo tu ni NECTA tosha..
 
mambo ya mitandao ni exposure ya mtu, hata wanaotumia kuna wale wa kushinda fb kwenye magroup ya ajabu ajabu, ukiona mtu anafika hadi JF basi level yake ya exposure ni nzuri, bado kuna wale ndugu zetu wa kuchanganya L na R
 
  • Thanks
Reactions: LA7
Back
Top Bottom