Sio kwamba najisifia la! hasha! Kuna wakati huwa natamani hata kaka yangu au dada yangu au ndugu wengine wa karibu waone au wasome nilichokiweka mtandaoni lakini inakuwa ngumu.
Katika familia yangu baba ana wanawake wa nne hivo watoto jumla tulio hai tupo 27, mimi ni wa 5 upande wa mama yangu katika watoto 8 na ndo mimi pekee yangu kwa familia yetu ninaye jua hata kutumia JF.
Lakini sababu inayochangia hawa ndugu wengine kuwa hivyo labda pia maisha ya kijijini kwa saana, ukiangalia pia mambo ya internet vijijini ni taabu japo si mimi pekee niliyetembea mjini.
mambo ya mitandao ni exposure ya mtu, hata wanaotumia kuna wale wa kushinda fb kwenye magroup ya ajabu ajabu, ukiona mtu anafika hadi JF basi level yake ya exposure ni nzuri, bado kuna wale ndugu zetu wa kuchanganya L na R