Mkoa gani hata ukipewa nyumba na gari hauwezi kuishi?

Mkoa gani hata ukipewa nyumba na gari hauwezi kuishi?

Tusiishi kwa kukariri watanzania wenzangu..Japokuwa mimi siyo mwenyeji wa Dodoma lakini nimejifunza kitu kwamba kila mkoa una fursa za ke bila kujali hali yake ya hewa...Mfano Dodoma watanzania wengi hawajui fursa nzuli zilizopo,,Dodoma ni mkoa ambao unaweza kulima kilimo chochote bila kutumia mbolea...Mahindi yanayolimwa Dodoma yanatoa unga mzuri sana maana hayatumii mbolea..Dodoma kunalimwa Alizeti,Zabubu,Karanga,Mihogo,Ulezi,Vitunguu,Nyanya,Mtama aina zote mweupe mpaka mwekundu,..Dodoma kuna ufugaji wa ng'ombe,mbuzi wanaozaa mpaka pacha 2,3 mapaka 4,Kuku wa kienyeji .....Kwa taarifa yako zabibu nizao pekee unaloweza pata mpaka shs milioni 9 kwa ekari sasa kinachofanya ushindwe kuishi Dodoma ni nini kama sio uvivu wako
 
We hujaona huu udhi kama una dharau?

So 900k ni pesa kubwa kiivyo?

Nimechukulia boda as general mtu anadharau unamuonesha dharau pia
Mkuu 900k ni pesa ndogo kwa mwezi?? Kwa mtu anayefanya kazi ya bodaboda?? Hivi umesahau kuna watumishi take home yao haifiki 500k??
 
Nilifika Lindi nikielekea Mtwara,pale njiani Ndandahimba sijui Tandahimba niliona vituko 😂😂😂.naona watu wanakimbilia baharini huko kila muda.
Nikauliza hawa wanaenda huko kufanya nini?
Si wakasema wenyeji huko chooni
Jamaa wanaenda kule wanabwaga kimba wanatimua,mawimbi yakija yanaondoka nayo duh nilichoka.
Lindi tukafika hakuna msosi palikua pa hovyo sana.
Fikiria stendi unakosa msosi zunguruka sana mpk tukatafuta taxi atuelekeze ndio kutupeleka nbc club at least tukapata supu kuku.
Mtwara kuna bar nafkiri inaitwa Pentagon ndo tulikua tunashinda hapo,walikua vizuri kwa menyu,huku mahotelini ilikua upuuzi mtupu, vichipsi tomato sauce kibao kipaja unapigwa buku 5.hela nyingi sana miaka hiyo
na ndio msosi wa maana utapata.
At least kwenye ile bar utakuta mbuzi choma , kuku choma, supu na vitu vingi tu.
Expirience yangu huko kusini.
Lindi jau kweli yani😅
 
Kuzuri balaa, fikiria mie nimeishi 1979 to 1984 lkn bado napakumbuka Sana pale regional block, katandala, sumbawanga wenyeji, Regina Mundi, chanji, izia, bangwe, jangwani, mazwi nk. Shule yangu Jangwani Primary school, ndugu zangu walisoma sumbawanga primary school na Mama yetu alifundisha hapo. Nakumbuka kanisa katoliki kila jpili tulikuwa hatukosi enzi za Bab askofu Kalolo Msakila alikuwa jemadari haswa. Nakumbuka ule uwanja wa zamani pale karibu na dimba la Nelson Mandera tulikuwa tunaenda angalia mechi kati ya Ujenzi na RTC, Ujenzi wakipigwa bao. Mdau fika uuone uzuri wa Sumbawanga!
Vaa barakoa mkuu
 
Mikoa yote iso na bichi siwezi ishi kwa hiari yangu.
 
Wakuu habari za weekend. Bila shaka ni shwari kabisa,

Kuna kitu nimewaza kuhusiana na harakati za utafutaji maisha na utulivu wa familia.

Niende kwenye maada husika mi nimebahatika kuishi baadhi ya mikoa hapa TZ bara na visiwani Pemba na Unguja nimeishi zaidi ya miaka 6 huko ukija bara Dar, Tanga, Atown, Tabora, Dom, Moro, Pwani, Shinyanga, Mwanza, Kilimanjaro, Sgd, kwa kuna Mkoa ambao hata nikipewa nyumba na gari siwezi kuishi ni Dodoma.

Yaani huo mkoa umekaa tofauti kabisa na sehemu nyingi nilizo ishi kuanzia kiuchumi, kijamii, kwa wale watumishi waliolenga kustaafia na kuishi huko hakika waishia kupauka na kunywa za pombe za kienyeji maana sioni future endelevu kabisa kwenye huo mjini na miongoni mwa miji yenye asili ya njaa uvivu na ukame kuna miji kama Tanga Moro au hata Mwanza unaweza ishi na familia bila tatizo tofauti huo mji wa Dodoma ambao wakazi wake wamekimbilia Dar na shughuli zao kwenye machinjio ya wanyama huko Vingunguti, Pugu na biashara ya Bucha

Ni wazi tunapambana na kwa ajili ya kujiandalia maisha bora ya sasa na baadae kwako na vizazi vyako hakikisha haukosei wewe pamoja na kukiweka kizazi chako jangwani kitateseka chagua sehemu sahihi ambayo itakufanya uishi kwa furaha. Kizazi chako ukikiweka jangwani kitashindwa kukusaidia hata wewe mzazi uzeeni.
Kanda ya kati yote, magharibi yote (rukwa, katavi, tabora n.a. kigoma) Mara, kagera tupa mbali kbsa
 
Mimi sijaona. Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar naweza ishi comfortable kabisa. Maisha yapo
 
Kigoma sijawahi kufika ila hunipeleki!
Kwakuwa huajawahi fika una haki ya kisema hivyo..hata mimi kabla sijafika nilikua na mtazamo kama wako..best place to live ina harmony.

#MaendeleoHayanaChama
 
Sijui kutofautisha kati ya net na gross ila nimekuambia mwisho wa mwezi kama hivi salio lazima lisome 900k sasa tofautisha kama ni gross au net.
Vilevile hata kama kazi yako ni kubwa kiasi gani usijaribu kudharau kazi ya mtu wapo watu wanafanya kazi for only150k per month lakini wanamiliki vitu ambavyo mtu anaepokea 300k/month hana. Hii social media huwa inatuwahadaa sana mpaka tunajisahau muda huo ukitoka online unakuta matatizo yako yamejipanga unashindwa hata uanzie wapi wapo watu humu hana uhakika wa kupata 100k kwa mwezi lakini huyo mtu ukimkuta anavyoidharau 900k humu JF utabaki unashangaa.
 
Back
Top Bottom