Mada hii itakuwa na 'Updates' za Uchaguzi Mkuu 2025 kama yanavyotujia kutoka kwenu kutoka mkoa wa Arusha. Ukiwa na taarifa yoyote ambayo ni ya eneo hili tafadhali usisite kuweka.
Mkoa wa Arusha una una jumla ya majimbo ya uchaguzi (7) ambayo ni
Arusha Mjini
Longido
Karatu
Ngorongoro
Arumeru Mashariki
Arumeru Magharibi
Monduli
Washindi wa Ubunge kwenye mkoa wa Arusha ni:
Mkoa wa Arusha una jumla ya Majimbo ya uchaguzi saba ambayo ni
1. Monduli - Isack Joseph Copriao (CCM) 2. Karatu - Daniel Awack Tlemah (CCM) 3. Arusha Mjini - Paul Christian Makonda (CCM) 4. Ngorongoro - Yannick Ikayo Ndoinyo (CCM) 5. Longido - Dkt. Steven Lemomo Kiruswa (CCM) 6. Arumeru Magharibi - Dkt. Johannes Lembulung’ Lukumay (CCM) 7. Arumeru Mashariki - Joshua Nassari (CCM)
Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Arusha Mjini ametangaza Paul Makonda kuwa mbunge mteule wa Jimbo la Arusha Mjini baada ya kupata kura laki tatu (300,000).
Tangazo hilo lilitolewa Oktoba 30, 2025 katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Arusha, ambapo Makonda, aliyegombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), alitangazwa mshindi wa kinyang’anyiro cha ubunge wa jimbo hilo.