Mkoa wa Kagera umebarikiwa kuwa na vyanzo vingi vya maji

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
4,869
Reaction score
13,137
Tanzania ni nchi kubwa kwa eneo na wachache pekee ndio wamepata fursa ya kuizunguka na kufahamu huku wengi wetu tofauti na mazingira yanayotuzunguka tumekuwa hatuna taarifa na uelewa wa sehemu nyingine za nchi yetu pendwa Tanzania.

Ni jukumu la Kila Raia wa Tanzania kwa nafasi yake kutangaza mazuri yanayopatikana nchini Tanzania sambamba na fursa za kiuchumi zilizopo eneo analoishi hii itasaidia kuwavutia wawekezaji kuja kuwekeza eneo husika na kuleta matokeo yenye tija kwa Taifa kama ajira na kodi kwa serikali.

Mimi naishi mkoa wa Kagera wilaya ya Missenyi napenda kuwafahamisha wale wote ambao hamjawahi kufika mkoa huu wa kaskazini magharibi mwa Tanzania kuwa huu ni miongoni mwa mikoa michache iliyobarikiwa kuwa na vyanzo vingi vya maji nchini Tanzania.

Na hilo ni kutokana na uwepo wa ziwa kubwa Africa ziwa viktoria na maziwa mengine madogo yanayopatikana katika wilaya za mkoa huu pamoja na mito na vijito vingi katika sehemu mbalimbali zilizofanya mazingira ya mkoa kagera kuwa kijani huku hali ya hewa ikiwa kati yaani si baridi wala joto.

Kama ilivyo sehemu yoyote yenye vyanzo vingi vya maji ni kuwa Fursa zinazopatika huko na mkoani Kagera zinapatikana kama kilimo Cha umwagiliaji, utalii na uvuvi.

From northern part of Tanzania.
 
Ni kweli hata wakazi wa mji ule wana maji ya kutosha nimekata kiu na nimetosheka ,dah yani nimemkumbuka ex wangu koku.
 
Sio fair hata kidogo kutoa Siri ya faragha na kuja Kufanya utani mbona vijana mnakosa shukrani
 
Ndio mkoa ambao hua nikiishiwa pesa nikizama miezi mitano napata pesa nyingi zaidi, nashukaga muleba, naenda mulumo nikichukua uduvi wangu miezi kama hii nikiutupa malawi au zambia tayari mtaji unajizaa mara mbili, napiga hadi nafika december kwenye maharage hadi mwezi wa kwanza nakua nshapata pesa ya kutosha narudi kula maisha mjini, kagera mmebarikiwa sana
 
Na wanangu wote wa kwenye maharage na viazi mviringo mbegu kutoka Rwanda, kyerwa na karagwe nabijuka muno
 
Ndio mkoa ambao hua nikiishiwa pesa nikizama miezi mitano napata pesa nyingi zaidi, nashukaga muleba, naenda mulumo nikichukua uduvi wangu miezi kama hii nikiutupa malawi au zambia tayari mtaji unajizaa mara mbili, napiga hadi nafika december kwenye maharage hadi mwezi wa kwanza nakua nshapata pesa ya kutosha narudi kula maisha mjini, kagera mmebarikiwa sana
Misimu miwili ya mvua na wakulima hawatumii mbolea lakini wanavuna mazao ya kutosha nakazia mkoa umebarikiwa.
 
Ndio mkoa ambao hua nikiishiwa pesa nikizama miezi mitano napata pesa nyingi zaidi, nashukaga muleba, naenda mulumo nikichukua uduvi wangu miezi kama hii nikiutupa malawi au zambia tayari mtaji unajizaa mara mbili, napiga hadi nafika december kwenye maharage hadi mwezi wa kwanza nakua nshapata pesa ya kutosha narudi kula maisha mjini, kagera mmebarikiwa sana
Kumbe fusa zipo mi nimejibanza kerebe tu
 
Mto Ngono, Mto Kagera, mto Kanoni, Kaja... kweli tumebarikiwa sana.
Kaja lile si ni tingatinga. Hivi kule hawawezi kulima mpunga maana maji ya kutosha na rutuba nyingi ila kuna tope sana. Wakiletwa wawekezaji lile tingatinga sijawahi ona mwisho wake nahisi linaweza toa mpunga tani laki kadhaa kwa mwaka
 
Ndio mkoa ambao hua nikiishiwa pesa nikizama miezi mitano napata pesa nyingi zaidi, nashukaga muleba, naenda mulumo nikichukua uduvi wangu miezi kama hii nikiutupa malawi au zambia tayari mtaji unajizaa mara mbili, napiga hadi nafika december kwenye maharage hadi mwezi wa kwanza nakua nshapata pesa ya kutosha narudi kula maisha mjini, kagera mmebarikiwa sana
Zambia wanakula uduvi? Maeneo mengi yanayozunguka ziwa Victoria wanautupa au kulisha mifugo
 
Tanzania ni nchi kubwa kwa eneo na wachache pekee ndio wamepata fursa ya kuizunguka na kufahamu huku wengi wetu tofauti na mazingira yanayotuzunguka tumekuwa hatuna taarifa na uelewa wa sehemu nyingine za nchi yetu pendwa Tanzania.

Ni jukumu la Kila Raia wa Tanzania kwa nafasi yake kutangaza mazuri yanayopatikana nchini Tanzania sambamba na fursa za kiuchumi zilizopo eneo analoishi hii itasaidia kuwavutia wawekezaji kuja kuwekeza eneo husika na kuleta matokeo yenye tija kwa Taifa kama ajira na kodi kwa serikali.

Mimi naishi mkoa wa Kagera wilaya ya Missenyi napenda kuwafahamisha wale wote ambao hamjawahi kufika mkoa huu wa kaskazini magharibi mwa Tanzania kuwa huu ni miongoni mwa mikoa michache iliyobarikiwa kuwa na vyanzo vingi vya maji nchini Tanzania.

Na hilo ni kutokana na uwepo wa ziwa kubwa Africa ziwa viktoria na maziwa mengine madogo yanayopatikana katika wilaya za mkoa huu pamoja na mito na vijito vingi katika sehemu mbalimbali zilizofanya mazingira ya mkoa kagera kuwa kijani huku hali ya hewa ikiwa kati yaani si baridi wala joto.

Kama ilivyo sehemu yoyote yenye vyanzo vingi vya maji ni kuwa Fursa zinazopatika huko na mkoani Kagera zinapatikana kama kilimo Cha umwagiliaji, utalii na uvuvi.

From northern part of Tanzania.
Infact... MashaAllah kona, directions na angles zote za Tsnzania zimebarikiwa..
Ardhi
Hali ya hewa
Moto,mistu
Maziwa bahari
Rasilimali watu,nk nk nk
 
Back
Top Bottom