Tetesi: Mkoa wa Mara kugawanywa

Hizi Bangi sasa huyu hajui anachosema na jiography ya wilaya za Tarime na Rorya hazijui ndio maana kaandika uharo huuu acha ujinga mrisya.
 
Wabaongeza mikoa ili wapate fursa za utawala huku ajira nyingine zikiwa bado kitendawili.

Any away, na sisi watu wa Majita tunataka mkoa wetu ambao makao makuu yake yatakuwa BUKIMA
 
Wengine wanaumiza kukuza uchumi wa nchi zao, kwenda anga za juu kuhangaika na chunguzi za kisayansi, kuongeza ajira n.k. sisi tunahangaika kugawa mikoa.
 
Mh Rais akipokuwa nzega ziarani Mh Mbunge wa nzega waliomba augawe Mkoa wa Tabora ili nzega iwe mkoa, Mh mbele ya ummati alikataa ombi hilo akasema serikali yake haina mpango kabisa wakuongeza mikoa wasahau
 
Huku tunakoenda hata makabila makubwa yatakuja kugawanywa nimestuka!


Sawa tu hata kama hayo unayoyaita Makabila yakigawanywa kwani yaliundwa na Mzungu, kabla ya Mzungu kuja hayakuwepo mahali yalipo na mengi hayakuitwa yanavyoitwa leo!
 
Ingegawanywa Morogoro
 
Nchi hii hakuna kinachoshindikana,kwani Mkoa wa Katavi una population ipi ya kuwa mkoa?
Kugawa mkoa kunaangalia vigezo vingi, kimojawapo ni ukubwa wa eneo husika sambamba na ulahisi wa utolewaji wa huduma za kiutawala.

Kwa mfano Katavi kabla haijaenguliwa kutoka Rukwa kulikuwa na maeneo mf. Tarafa ya Karema ni kilometa 350 kufika makao makuu ya mkoa yaani Sumbawanga,baadhi ya maeneo ya mwese na mishamo ni kilometa hadi 400 ili kufika makao makuu ya mkoa.sababu kama hizi pia huangaliwa katika kusogeza huduma za kiutawala kwa wananchi.Tusibeze kila kitu.
 
Ugawanywe tuu, ni eneo kubwa sana kijiografia, kama katavi, ambayo ni wilaya ya mpanda tu,si no sawa na Tarime tu kuwa mkoa
Kugawa mkoa kunaangalia vigezo vingi, kimojawapo ni ukubwa wa eneo husika sambamba na ulahisi wa utolewaji wa huduma za kiutawala.

Kwa mfano Katavi kabla haijaenguliwa kutoka Rukwa kulikuwa na maeneo mf. Tarafa ya Karema ni kilometa 350 kufika makao makuu ya mkoa yaani Sumbawanga,baadhi ya maeneo ya mwese na mishamo ni kilometa hadi 400 ili kufika makao makuu ya mkoa.sababu kama hizi pia huangaliwa katika kusogeza huduma za kiutawala kwa wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…