Tetesi: Mkoa wa Mara kugawanywa

Tetesi: Mkoa wa Mara kugawanywa

Mara nzima ina watu laki nane kwahiyo kila mkoa utakua na watu laki nne nne oky sio mbaya
Mara Region is one of Tanzania's 30 administrative regions. The regional capital is the municipality of Musoma. According to the 2012 national census, the region had a population of 1,743,830, which was lower than the pre-census projection of 1,963,460.[1] laki nane umeitoa wapi mkuu?
 
Yanajitafutia ulaji. Mkoa unaopaswa kugawanywa kwa sasa hivi ni Tabora na ndio mkoa pekee uliobaki na eneo kubwa! Hii mingine ni maigizo tu. Yaani unagawa mikoa wakati nchi ina baa la njaa?
 
Mkoa wa Mara hauwezi kugawanywa maana Kijografia ni miongoni mwa mikoa minne yenye maeneo madogo ya nchi kavu Tanzania ikiwa nyuma ya Mtwara na Kilimanjaro na Dar.

Eneo kubwa la mkoa limemezwa na hifadhi ya Serengeti na Ziwa Victoria, na total surface area iliyopo ni kama 19,566 sq. kms.

Kwa population ya 1.7 Milions kulingana na sensa ya mwaka 2012 mkoa wa Mara ni mmoja ya mikoa yenye density ya mifugo kubwa sana na road density kubwa mno, kwa hiyo kuukata maana yake unaunda migogoro mipya ya ardhi na mapigano ya kikabila yasiyoisha hasa kutokana na kuwa na makabila makubwa ya wakulima na wafugaji kama Wakurya.

Kuugawa mkoa huu ni kuuvuruga tu kwani hata maendeleo yake si makubwa kihiivyo.
 
Kugawa mkoa kunaangalia vigezo vingi, kimojawapo ni ukubwa wa eneo husika sambamba na ulahisi wa utolewaji wa huduma za kiutawala.

Kwa mfano Katavi kabla haijaenguliwa kutoka Rukwa kulikuwa na maeneo mf. Tarafa ya Karema ni kilometa 350 kufika makao makuu ya mkoa yaani Sumbawanga,baadhi ya maeneo ya mwese na mishamo ni kilometa hadi 400 ili kufika makao makuu ya mkoa.sababu kama hizi pia huangaliwa katika kusogeza huduma za kiutawala kwa wananchi.Tusibeze kila kitu.
Kama ni hivyo mbona kagera haigawanywi maana kutoka ngara hadi makao makuu BUKOBA km 400,biharamulo km300 na kyerwa 165 mbona mkoa haugawanywi mi sijui wanatumia vigezo gani?
 
Tuangalie mapato yao kama wataweza kuendesha mikoa 2 na pia idadi ya watu......kuna haja kweli kwa sasa serikali ina strugle na mapato big time!!!
 
Kuna taarifa ambazo bado ni tetesi kuwa Mkoa wa Mara unategemea kugawanywa na kuwa mikoa miwili, Taarifa zinasema, kutakuwa na Mkoa wa Mara kaskazini na Mara kusini, hali kadhalika, wilaya kadhaa zitaongezeka ili kukidhi mahitaji ya kimkoa.

Taarifa zinadai kuwa, Makao makuu wa Mkoa mpya wa Mara kaskazini yatakuwa UTEGI ambapo kutakuwa na wilaya kama RORYA, SHIRATI, TARIME, SIRALI na Nyamongo, hivo hivo, Mkoa mpya wa Mara kusini utabaki na wilaya zake kama Msoma mjini, Butiama, Serengeti, na wilaya zingine.

Haijafahamika mara moja nia na dhumuni la kuugawa huu mkoa, ila kwa maoni yangu, sioni sababu ya kuugawa huu mkoa.
Bunda itapelekwa wapi??
 
Kwanza ifahamike kuwa mtoa post ni Muongo na Mpotoshaji mkubwa Kwa sababu hawawezi kugawanya Mkoa mdogo kama ule wakaacha Mkoa wa Tabora, Singida na Morogoro!

ii) Tetesi zilizokuwepo tangu mwaka 2014 ni kwamba Kisiwa cha Ukerewe kilitakiwa kurudishwa Mkoa wa Mara hadhi kufikia mwezi wa 7, 2015. Sio kugawanya Mkoa!!.
Hii ilitokana na Ugomvi wa Vivuko chini wa Wizara ya Ujenzi ambapo ilikuwa ikongozwa na Waziri Magufuli JP na Nadhani iliathariwa na Uchaguzi Mkuu wa 2015 baada ya Magufuli Kuteuliwa kugombea Urais wa Tanzania. Mpaka sasa hivi naona wamekaa kimya hakuna utekelezaji wake! Sababu zingine ni Ukaribu kati ya Ukerewe na Mkoa huo na Utata wa Upokeaji wa Mishahara kwa Watumishi wa Serikali hasa wale wanaofanya Kazi Visiwani kama vile Irugwa, Bukara,Rwegoba n.k!

Dogo acha kutafuta kiki!
 
Mtu anakurupuka anaweka uongo wake humu udio na chanzo anauweka humu watu wanaanza kuchangia.
Yaani mtoa mada anashindana na Godbless Lema kuota ndoto za kusadikika.
 
Kuna taarifa ambazo bado ni tetesi kuwa Mkoa wa Mara unategemea kugawanywa na kuwa mikoa miwili, Taarifa zinasema, kutakuwa na Mkoa wa Mara kaskazini na Mara kusini, hali kadhalika, wilaya kadhaa zitaongezeka ili kukidhi mahitaji ya kimkoa.

Taarifa zinadai kuwa, Makao makuu wa Mkoa mpya wa Mara kaskazini yatakuwa UTEGI ambapo kutakuwa na wilaya kama RORYA, SHIRATI, TARIME, SIRALI na Nyamongo, hivo hivo, Mkoa mpya wa Mara kusini utabaki na wilaya zake kama Msoma mjini, Butiama, Serengeti, na wilaya zingine.

Haijafahamika mara moja nia na dhumuni la kuugawa huu mkoa, ila kwa maoni yangu, sioni sababu ya kuugawa huu mkoa.
Muda si mrefu kila kata itakuwa wilaya.
 
Siasa mbele ya taaluma mbona wilaya kite to ni kubwa kuliko mkoa Wa Kilimanjaro? Toka mkoa Wa manyara ugawanywe toka Arusha nilitambua kipaumbele ni upuuzi sio geographical area wala population
 
Kwanza population itatosha ?

hivi ili mkoa uwe mkoa wanajua unahitaji population ya watu wangapi?

Wanapanua tu matumizi baada ya kubana matumizi shame on you........

Vigezo vya kugawa maeneo ya kiutawala view reviewed.
Hili suala LA population naona huwa linachukuwa nafasi kubwa but kwa maoni yangu kuna maeneo hili lisiwe LA mkazo sana kwani changamoto ni nyingi
Mtazamo wangu binafsi maeneo mengi yaliyopata hadhi za mikoa, wilaya miaka ya karibuni ni kwa sababu Tu yalipata mzito wa kubeba hiyo agenda au zababu za kisiasa.
Yapo maeneo unakuta ni wilaya ila kubwa kuliko baadhi ya mikoa.
 
Kwanza population itatosha ?

hivi ili mkoa uwe mkoa wanajua unahitaji population ya watu wangapi?

Wanapanua tu matumizi baada ya kubana matumizi shame on you........
This can't be true.How on hell can the government and CCM do that.This will be extremely poor timing on the part of CCM.To me CCM needs to do only those things which will benefit and impress the wananchi."Unless this is in preparation for the 2020 elections."
 
Mzee wa kubana matumizi hatakubali. Aidha hiyo clip ya mwanamke wakamatwe wote mara moja. huu ni udhalilishaji wa kupindukia. hata kama kakosea si kipiga.
 
Back
Top Bottom