Wakuu Mimi niko mkoa wa Mara huku sirari mpakani na Isibania jirani kabisa na Kenya.
Kwa utafiti Wangu Mkoa huuu wagombea wa CCM kwenye majimbo yote wana kazi ngumu sana kuliko mikoa yote hapa Tanzania katika Uchaguzi wa 28, October.
Ukitizama kila jimbo wagombea wa Chadema wana umaarufu kuliko wagombea wote wa CCM, halafu wagombea wote wa chadema wanajua siasa usisema wanajua kucheza na jukwaaa, wanaongea utadhani walisomea kuongea na ni wazuri hadi huko bungeni.
Na ukisikiliza wananchi kila mtu anamsifia mgombea wa Chadema na wanajiuliza kwanini CCM haijatafuta watu wanaoweza kuongea? Kiukweli wagombea wa Chadema mkoa wa Mara ninawapa salute, na sioni ni namna gani CCM itashinda kwenye majimbo ya mkoa wa Mara.
Watu wachache wanasema kuwa Mwita waitara anakaribia kwa mbaaaali kutoa sauti kwenye jukwaaa ila wanadai tatizo lake anaongea kwa kuwafokea na huwa wanahis kama sio mtu sahihi kuwa mwakilishi wa wananchi hasa kutokana na muonekano wake alivyo ingawa muda mwingi anakuwa hajanywa pombe ila watu huhis kuwa muda wote amelewa, tatizo watu hapa hushinda Kuelewa kuwa ule ni mwonekano tu wa kwake.
Lakini kwa majimbo mengine wagombea wa CCM hawawezi kumiliki jukwaaa na inaonesha kuwa kama Uchaguzi utakuwa wa huru na haki majimbo yote yataenda Chadema.