Mkoa wa Mbeya una haya madini ya pesa nyingi sana

Mkoa wa Mbeya una haya madini ya pesa nyingi sana

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
11,884
Reaction score
21,175
Panda Hill

Kuna haya madini yanaitwa Niobium. Yanatumika kwa kuchanganya na chuma ili kukifanya kiwe imara na kitumike kwenye vitu kama ndege, vifaa vya anga za juu, vifaa vya kivita na vifaa vyote vinavyohitaji chuma imara. Kwa sasa Brazil ndiye mzalishaji mkubwa wa madini hayo, akizalisha asilimia 80 ya mahitaji ya dunia. Brazil wana tonne milioni 800 za mawe yenye madini ya niobium.

Kwenye eneo la Panda Hill, karibu na uwanja wa ndege wa Songwe, Mbeya kuna deposit kubwa sana ya madini ya Niobium. Kuna mawe yanayokaribia tani milioni 178 yenye 0.5% Niobium Oxide. Kwa hiyo kuna karibu tani laki tisa za madini ya niobium.

Tani moja ya madini haya ni kama dola 40,000 au Tsh milioni 100 hivi. So value ya madini yaliyopo hapo Panda Hill ni kama dola bilioni 36 au Tsh trilioni 94

Mahitaji ya sasa ya niobium duniani ni tani laki moja kwa mwaka.

Mwaka huu mwanzoni serikali imeingia mkataba wa kuzalisha madini hayo. Imepokea dola milioni 300 na 16%. Mradi unategemea kuzalisha kwa kuanza kiasi cha tani 1800 kwa mwaka, kwa miaka 24. Madini hayo yatakayozalishwa yana thamani kama ya dola milioni 72 kwa mwaka. Uzalishaji huu tu unaenda kuifanya Tanzania kuwa mmoja wa wazalishaji wakubwa wa madini haya duniani.

Ngualla Hill.

Kuna haya moja ya madini adhimu yanayoitwa Neodymium. Madini haya yanatumika kutengeneza sumaku zenye nguvu sana. Sumaku hizi zinatumika kwenye magari ya umeme, vifaa vya electronics(Vibration za simu, speakers za simu, airpods nk), yanatumika pia kwenye mitambo ya kuzalisha umeme wa upepo.

China ndiyo ina kiasi kikubwa cha madini hayo kwa wingi duniani. Ikikadiriwa kuwa na tani 44 milioni ya Neodymium Oxide. Tanzania ni ya nane ikiwa na tani laki tisa. Kiasi chote hicho kinapatikana kwenye mlima Ngualla uliopo kama km 150 kutoka mjini Mbeya(Kwa sasa Ngualla ni mkoa wa Songwe). Mwamba huo una tani milioni 200 zenye madini adhimu ikiwemo Neodymium.

Gharama ya madini ya Neodymium Oxide ni dola 100 kwa kilo. Hizo tani laki tisa ni dola bilion 90 au Tsh trilioni 237.

Wachimbaji wanataka kuanza na mwamba wenye madini mengi ambao utatoa kama tani laki mbili za Neodymium zenye thamani ya kama dola bilioni 20. Madini haya ya Neodymium yamegunduliwa pia mwaka huu huko Ludewa na pia yamepatikana huko Kilosa.

Mahitaji ya dunia ya madini ya Neodymium ni kama tani 60,000 kwa mwaka.

Mahitaji ya madini haya mawili, Niobium na Neodymium yanakua kwa kasi sana sababu teknolojia ya dunia inakokwenda inayahitaji sana.

Kama nchi tufanye nini tunufaike na utajiri huu?
 
Back
Top Bottom