Boss ni Mwanza ipi unayosema Mwanza ya Somalia, Karagwe, Mpitimbi, Dareda , Malinyi au Kibondo? kwani Mwanza we umewahi kufika au umeona picha tu za mnara wa samaki kwenye mji mdogo unaoitwa Jiji?
Mwanza ina Barabara za maana mbili tu Kenyatta na Nyerere!! mji mzima magari yanazigombania!!
Barabara muhimu za kuunganisha mji kupunguza foleni na kujivunia jiji zote bado ni za vumbi tangu ukoloni
mfano
1.Kisesa to Buhongwa kupitia Kakebe sijui machinjioni huko kwenda kanyerere sijui Maina hadi kuungana na Kenyatta road kwenda Buhongwa na Nyashishi ni mavumbi tu yanatimka na mashimo tu lami haina tangu ukoloni sidhani kama hilo eneo lina mbunge mwenye akili au nia ya kujali watu waliozoea kula mavumbi!!
2. Barabara kutoka Butimba kona kwenda Sweya ni muhimu ila ni ya mavumbi matupu na mashimo lami hamna tangu ujima
3. Barabara kutoka Kisesa kwenda Kayenze ni ya muhimu kuelekea visiwani nayo ni ya mavumbi na mashimo lami haina tangu uhuru
4. Barabara ya Kutoka Airport kwenda Igombe ni mavumbi matupu na mashimo lami haina
Binafsi huwa sielewi na nachukia Mwanza kuitwa Jiji maana sijui ina vigezo gani vya kuitwa Jiji!!
Mavumbi yanatimka tu mji mzima!! Barabara ni mbili tu za lami!
Hali ni ngumu sana viwanda hakuna business kubwa ni dagaa na samaki tu tena vina msimu!
Mji mzuri kutokana na ziwa ila hauna miundombinu ya utalii wazungu wa kuhesabu!
Hebu wahusika wa Tanroads oneni aibu wekeni lami Feeder Roads zote mji ufanane kuitwa Jiji