Mkoa wa Pwani unagawa kwa Wafugaji maeneo ya kufugia(Min Ranch)

Joined
Jun 26, 2026
Posts
7
Reaction score
24
Huu ni mpango wa mkoa wa Pwani kugawa maeneo ya uwekezaji kwa ajili ya kufugia na kulima malisho(Min Ranch)ambapo kila mfugaji au mfugaji mtarajiwa atapewa ekari 125 sawa na hekta 50.

Masharti ni kufuga na kupanda malisho si kwa ajili ya kilimo, lengo likiwa kupata mashamba ya kisasa ya mifugo ambayo wafugaji watafuga kisasa bila kuhamahama .

Mpango huu ulianza miaka michache iliyopita lakini tarehe 19 Juni 2026 mkuu wa mkoa wa Pwani Mh. Abubakar Kunenge aliulezea kwa kirefu mbele ya Waziri mkuu Mh.Dr.Mwigulu Nchemba wakati wa ufunguzi wa mnada na maonesho ya mifugo ya Tri nations yaliyofanyika Mbogo Ranch Ubena Zomozi mkoa wa Pwani.

Mpango huu unaenda kuhamasisha ufugaji wa kisasa,ulimaji wa malisho na matumizi ya teknolojia za kisasa katika ufugaji.

kupata habari hizi kwa kirefu na habari nyingine za kilimo na ufugaji tembelea page ya Instagram ya africa_kilimo_news_

Humo utapata habari zote kuhusu yaliyojiri wakati wa maonesho ya mifugo kanda ya ziwa yaliyofanyika Shinyanga tarehe 30-31 Mei 2026,Maonesho ya siku ya ubunifu na teknolojia katika sekta ya maziwa yaliyofanyika TALIRI Tanga tarehe 11 Juni 2026 na Mnada na maonesho ya mifugo ya Tri nations yaliyofanyika Mbogo Ranch tarehe 19-21 Juni 2026.

IMG-20260804-WA0002.jpg
IMG-20260804-WA0003.jpg
 
View attachment 3643168View attachment 3643171
Process zikoje kuomba hayo maeneo,masharti na ada kama zipo
 
Pwani itaenda kugeuka jangwa soon
Siyo ufugaji wa kuzurula kila mahali na mifugo.
Unakuwa na shamba la mifugo unalima nyasi. Unaweka vizimba vya kulishia vinakuwa na uzio (fence).
Unakuwa na maji ya kumwagilia na kunywa wanyama.
Unalima nafaka za kula wanyama.
Unatunza haystack n.k.
Mfano shamba la huyo Mbogo ranch huko Chalinze Pwani, au Asas dairy wa Iringa wana ranch yao.
 
Back
Top Bottom