kiwatengu
Platinum Member
- Apr 6, 2012
- 18,585
- 16,780
Wakuu mambo vipi?
Mimi ni mzaliwa wa Wilaya ya Misenyi mkoa wa Kagera, Kijiji cha Rusinga! Pia Nsunga ni kwetu.
Nimekulia mkoa wa Kilimanjaro so Naifahamu Kagera vizuri na Naifahamu Kilimanjaro vizuri sana.
Hoja yangu naileta kutokana na Spika Ndugai jana kutuzodoa wana Kagera kuwa hatuna kitu tena yale mambo ya Nshomile hakuna tena, akadiriki kabisa kutufananisha na Dodoma kwao.
Alinifanya niutafakari vizuri huu mkoa wangu ninaoupenda na kulinganisha na alichokisema, Hatuna chuo Kikuu hata kimoja mbali na Open University.
Nini kisababishi? Mbona mkoa wetu wa Kagera umetoa wasomi wengi ukilinganisha na Mkoa wa Kilimanjaro ambao kijiografia ni mdogo sana?
Maprofesa waliotoka Kagera ni wengi, nini kilikwamisha uwekezaji wa Elimu Kagera? Kama ni maeneo tunayo yakutosha mandhari nzuri na zakuvutia wenyeji mnajua, hali ya hewa ni safi sana. Ukiwa Biharamulo kwenda Muleba, ukija mpaka Bukoba Rural, Misenyi, Kyerwa, Karagwe na Ngara mazingira ni mazuri sana.
Huwa naifurahia sana hali ya hewa ya kijijini kwetu Rusinga walikozikwa mababu zangu.
Tuwekeze kwenye Elimu kwani ndio sehemu/kitu wana Kagera wanaweza kukifanya kwa ufanisi wa hali ya juu.
Vilevile tunapopata fursa hasa tunapokuwa kwenye vyombo vya maamuzi tusisahau kwetu. Mheshimiwa Byabato kama uko huku jukwaani please! Kwasasa tu privilege mkoa wetu tuepuke kunangwa nangwa na kina Ndugai.
Kaka Bashungwa hebu fanyeni namna kuendeleza Kagera yetu, Kielimu na miundo mbinu.
Hivi mnajua Kilimanjaro wao wanashule na vyuo kibao? Na isitoshe hata miundo mbinu yao mingi iko vizuri. Makao makuu yote ya wilaya zao zimeunganishwa kwa lami.
Hata sisi tunaweza kukijipa kipaumbele,pia watu mnaowapa connection wahamasisheni wakajenge kwao Kagera.
Ndugu yangu Mhe. Mhandisi Ezra John Chiwelesa Ipambanie Biharamulo maeneo yapo yakutosha tafuta wawekezaji kipaumbele kiwe elimu
Steven L. Byabato nimeshakusemea hapo juu Bukoba must Change!
Bukoba Vijijin inakutegemea sana Bwana Rweikiza Jasson. Hamasisha uwekezaji wa Vyuo.
Kule Kyerwa Mheshimiwa Innocent Sebba Bilakwate. Shirikiana vizuri na Bashungwa Karagwe na Kyerwa ziendelee sana.
Waheshimiwa wa Muleba Kazkazini na Kusini inapaswa kupaa kimaendeleo, msiendelee kuchelewa.
Mheshimiwa Ndaisaba Ruhoro Ngara bado iko nyuma sana kimaendeleo amkaa.
Mbunge wangu wa Nkenge Mheshimiwa Florent Kyomo sijui utafanyaje but Nkenge na Misenyi yote wanatakiwa kuendelea.
Kingine tujenge utamaduni wa kwenda kwetu mara kwa mara pamoja na familia zetu. Uwe utaratibu wa kwenda nyumbani walau mara moja kwa mwaka, hii itachochea mabadiliko tupeleke na watoto wetu wakajionee Mkoa wao na Mazingira yao yalivyo mazuri.
Asanteni kwa kunisikiliza.
Naipenda Kagera, Naipenda Kilimanjaro, Naipenda sana Tanzania.