Mkuu angalia dalili zifuatazo kama unazo ndo ujue una tezi dume..afu pia tezi dume wengi inawaaffect wazee wa 50's..
1) Kupata shida wakati wa kuanza kukojoa.
2) Kutiririka kwa mkojo baada ya kumaliza kukojoa.
3) Kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu.
4) Kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku.
5) Kujikakamua wakati wa kukojoa na kushindwa kumaliza mkojo wote
6) kutoa mkojo uliochanganyika na damu.
Pamoja na kueleza dalili hizo watu wanapashwa kutambua kuwa, mwanaume anapoanza kuona na kuhisi baadhi ya dalili hizo, anapaswa kujua kuwa, seli za saratani katika tezi dume lake huwa zina umri wa takribani miaka saba na kuendelea.
Iwapo saratani imesambaa mwilini kiasi cha kuhusisha sehemu nyigine za mwili, mgonjwa anaweza kuwa na maumivu makali ya mifupa katika maeneo ya nyonga, mapajani na kiunoni.
Aidha mgonjwa huwa na dalili nyingine zinazoweza kumpata mgonjwa mwingine yeyote wa saratani kama vile kupungua uzito, kuhisi kichefuchefu, uchovu, kizunguzungu na kadhalika.
Pia angalia sperms zako kama zinatoka zikiwa zimechanganyikana na damu...