Uchunguzi wa awali kwenye Hospitali ya Wilaya ya Kinondoni, Mwananyamala, umeonesha kwamba Mkoloni aliwekewa vitu vinavyofanana na madawa ya kulevya kwenye 'mtori' aliokunywa pale Meeda Bar, Sinza. Lakini habari zaidi zinasema kwamba hayo yalithibitishwa alipohamishiwa Muhimbili, ambapo madaktari walimtibia mpaka alipoanza kupata nafuu. Hata hivyo, baada ya kupata nafuu hiyo na kuzinduka, alishindwa kuona sawa sawa, akawa anaona kila kitu mara mbili. Tunatarajia mpaka kesho, kijana wetu, shujaa wetu, atakuwa amerejea katika hali yake ya kawaida.
Walichotaka - mafisadi hawa - ni kummaliza, kwani wanajua nguvu yake na umahiri wake kisanii. Ukweli ni kwamba Wagosi wa Kaya wana ushawishi mkubwa sana kwenye uwanda wa siasa, kutokana na historia yao ya muda mrefu ya kuikosoa Serikali na mafisadi wote, kwenye tungo zao nyingi ambazo zilipendwa kutokana na ujumbe uliokuwa na hisia kali.
Hizi ni hujuma za kuwatisha wasanii wasishiriki kwenye ushawishi wa kisiasa kwenye kambi ya upinzani. Lakini nasema wamechelewa, wamechelewa MNO!
HATUTISHIKI! HATUDANYANYIKI! UKIFA SHUJAA MLANGO WA PEPO NI WAKO!
Niko tayari kufa kwa kuitetea nchi yangu!
-> Mwana wa Haki
P.S. Ninamfahamu Mkoloni. Ni kweli, hii sasa ni criminal case. Wahusika wote wa MEEDA BAR wako chini ya ulinzi wa polisi. Kesi zote za kujaribu kuua HAZINA DHAMANA! Watawekwa ndani mpaka kieleweke! Na WATAWATAJA waliowatuma!