Elections 2010 Mkombozi Slaa apokelewa kwa kishindo Kahama

Elections 2010 Mkombozi Slaa apokelewa kwa kishindo Kahama

Dah! Huu utitiri wa watu unatia moyo. Hakika mwaka huu ni mwaka wa mabadiliko.
 
Wachakachuaji na mabwana zao wameshika tama. Ngoma ya kuchakachua imeonekana itakuwa nzito! You WACHAKACHUAJI, you would better give up now and do something sensible and productive to NJI HII than later!

Go Dr. SLAA, Gooooooooooooooooooooooooo!
 
].... hakuna haja ya kutembea na wasanii na wengine wanaume wamevaa gauni ili kupata watu wa kuhutubia. Wananchi wanahaja ya kujua mustakabali wa nchi yao na sio mbwembwe za wasanii. Huko ni kufirisika kifikra. Hata Mwalimu Nyerere wakati anadai ukombozi wa nchi hii hakuwa na wasanii bali hoja za msingi kwa Watanganyika.[/B]


CHAGUA CHADEMA!!!!



Nimeipenda hiii!
 

Wadau;

Habari nilizopata kutoka rafiki yangu aliye Kahama anasema Dr mkombozi wetu amepata mapokezi makubwa mjini humo jana (Jumapili) ambayo hayapata kutokea hapo.



Anasema ingawa alichelewa kidogo na kutinga saa 11.15 jioni umati mkubwa ulikuwa bado unamsubiri katika uwanja huo na alikwenda moja kwa moja jukwaani. Vifijo, vigelegele na vifijo, vikiambatana na kelele za BYE BYE KIKWETE, BYE BYE CCM zilisikika wakati anaingia.

Akihutubia alisikitishwa na manyumba duni (ya tembe) ambayo wananchi wengi bado wanayo baada ya miaka hamsini ya ‘maendeleo' yanayodaiwa kuletwa na CCM.

Alisema watu ni masikini sana wilaya hiyo pamoja na kwamba wanakalia eneo la migodi miwili mikubwa ya dhahabu – Bulyanhulu na Buzwagi. Alishangaa kwa nini kila mgodi katika hiyo inachangia sh milioni 200 tu kila mwaka kwa hakmashauri ingawa kila mmoja unapishana katika uzalishaji.

Alisema tofali moja (gold bullion) la tofali la dhahabu lingeweza kusomesha watoto wa wilaya hiyo bure kuanzia shule za msingi hadi chuo kikuu.

Alimshambulia JK kwa kutoa ahadi za uongo zisizokuwa na mantiki. Alisema JK anapotoa ahadi kwamba atatengeneza barabara anadanganya tu, kwani kazi ya serikali ni kutengeneza barabara kwa sababu ndiyo inakusanya kodi. Alishangaa kuona kwamba JK anaifanya hiyo kuwa ahadi ya kampeni. Slaa alisema hivyo huku wananchi wakimshangilia kwa nguvu.

Awali alipokuwa maeneo ya vijijini, wananchi walikuwa wanamzuia barabarani ili awaslimie na awahutubie na alikuwa anafanya hivyo, ndiyo maana ya kuchelewa mkutanoni.

Kuhusu mgombea wa ubunge, rafiki yangu huyo alisema mgombea wa CCM, James lembeli yuko katika hali mbaya sana na dalili kubwa ni kwamba atapoteza kiti hicho kwa yule wa Chadema.

Rafiki yangu anasema Lembeli amekonda sana shauri ya mawazo ya kushindwa ingawa yeye anasema atashinda tu kwani kukonda kwake siyo sababu.

Hali kadhalika mgombea wa CUF katika jimbi jirani la Msalala naye amemkalia vibya mgombea wa CCM – Maige na dalili ni kwamba atakipoteza kiti hicho.

====
UPDATES - PICHA

slaa_in_kahama.jpg

bango_nzega.jpg

bango_salma.jpg

slaa_nzega_kahama.jpg


Kazi ni kupiga, kulinda, kuhesabu na kujumlisha kura kwani hapo ndipo mafisadi wamejipanga kuwapora wananchi na kuendeleza utawala wa baba, mama na mtoto. Ni lazima kujipanga kuepusha hayo.
 

Heshima kwako Nyumbu,

Mkuu Mlingwa ni rafiki yangu wa karibu sana tangu akiwa mkurugenzi TAWIRI.Kwasasa Mlingwa yuko Njiro[Msolla] nyumbani kwake anasoma magazeti tangu asubuhi mpaka jioni mambo yake si mabaya sana ana Landrover moja anaitumia kwa shughuli za utalii si unajua tena Arusha watalii wengi kipindi hiki.

Mlingwa anategemea kujiunga Sokoine University kama mwalimu mwakani uongo mbaya elimu yake nzuri hawezi kulala njaa lakini inataka moyo from deputy minister hadi mwalimu !,siasa wakati mwingine inaweza kukuangusha vibaya hadi mbwa unaowafuga wakakudharau.

Jamani tusishangae Dr. Mlingwa kwenda kuwa Mhadhiri pale SUA ndo jambo la msingi na atakuwa amefanya uamuzi mzuri sana mimi namuunga mkono kwa hilo. Mbona Al Gore alirudi chuoni kufundisha? Leo tushangae kwa Dr. Mlingwa kwenda kufundisha Chuo Kikuu?
 
Back
Top Bottom